Kinachosikitisha ni kwamba Watanzania tulikuwa mstari wa mbele kusaidia wenzetu katika ukombozi barani Afrika kiasi kwamba hata Waganda tuliwaondolea kadhia ya dikteta Idi Amin lakini leo tunamlea wa kwetu. Tunashangilia ndugu zetu wakipigwa, kulemazwa na hata kuuawa na vyombo vyetu vya usalama tunaowalipa kutulinda.
Ndugu zetu wanakamatwa na kuteswa na wale wawakilishi tuliowachagua wenyewe tunafurahi wakinyanyaswa na viongozi uchwara wa kuteuliwa. Hivi leo Idi Amin angekuwa hai tungekuwa tunamwimbia nyimbo za kumsifia na bila shaka tungeshampokea kwa vifijo akifanya ziara hapa kwetu kama tunavyowapokea madikteta waliotuzunguka.
Whither to? Tunaelekea wapi ndugu zangu? Tulimpinga mkoloni ndani na nje ya mipaka yetu, tuliwalaani wakoloni weusi kama Bokasa na Nguema...lakini leo tunawapigia makofi Museveni, Shein na Nkuruzinza. Tunashangilia ndugu zetu na majirani wakiwashughulikia wanaotofautiana nao kimawazo na sasa yanaanza kutupata.
Katiba inasiginwa kwa kisingizio cha eti kunyosha nchi na tunapiga vigelegele. Watu wanapotea katika mazingira ya kutatanisha huku tukiimba hapa kazi tu. Wakati wa Idi Amin ilifikia hadi mamba ziwani victoria walikula nyama za watu hadi kukinai na maiti zilizowazunguka zikielea wakawa wanazitazama tu...so sad!
[HASHTAG]#freemaxcencemello[/HASHTAG] now!