Quran na uislam zilipishana wapi na kwanini??

Na mkristo aliyesoma sana biblia anafungua kanisa na kupiga hela.

haha natania tu mkuu.
 
Hawa wanaochukizwa na ugaidi humu ndiyo wengine wanashabikia vita,sasa sijajua kwanini ugaidi uwachukize lakini washabikie ugomvi wa N.korea na Marekani?
 
Swali
Ivi haya makundi ya Siasa kali kama ISIS yakifaniliwa kuiteka dunia na kuitawala,
Hali itakuwaje ?
Naomba jibu.
 
Swali
Ivi haya makundi ya Siasa kali kama ISIS yakifaniliwa kuiteka dunia na kuitawala,
Hali itakuwaje ?
Naomba jibu.
Duh! we unaamini kabisa hayo makundi yana dalili ya kuteka dunia? na unaamini kabisa hao wakubwa wa dunia wamewashindwa?
 
Hakuna anayepotosha dini, viongozi wa waislam wanatakiwa wakemee vitendo vya kigaidi, ili watu wote wajue kwamba dini ya Kiislamu haina mafundisho ya kigaidi.
Tambua kwamba viongozi wa kupandikizwa wamejaa kibao...kwa zama hizi kuna viongozi wanaopotosha na wapo ambao wanaiendeleza dini hii kwa haki na kuielimisha jamii kwa usahihi....uislamu hauna historia ya kigaidi na ugaidi hauna nafasi katika uislamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmmh
 
55. Pale Mwenyezi Mungu alipo sema: Ewe Isa! Mimi nitakufisha, na nitakunyanyua kwangu, na nitakutakasa na wale walio kufuru, na nitawaweka wale walio kufuata juu ya wale walio kufuru, mpaka Siku ya Kiyama. Kisha marejeo yenu yatakuwa kwangu, nikuhukumuni katika yale mliyo kuwa mkikhitalifiana.

Shida katika uislamu na hayo yote uliyoyataja mleta mada ipo ktk tafsiri ya quran miongoni mwa viongozi wa waislamu ndio shida zote zinapoanzia na vurugu zote

Mfano hiyo aya hapo juu ambayo ipo ktk Suurat Al I'imran kwenye hiyo aya Ahmadiya wana tafsiri yao ambao wao wanakiri kuwa Issa ni kweli alikufa kama Allah alivyosema atamfisha ukija kwa wasunni na washia wanakataa tena wakiwaita ahmadiya ni makafiri kwa kukubali Issa alikufa kama wakiristo wao wanasema Issa hakufa ila Allah alimuepusha na kifo na kumpeleka sehemu salama

Kwa mfano huo utaona shida kubwa ndani ya uislamu ni tafsiri ya maandiko yao wao wenyewe na hivyo kupelekea matatizo
 
kwa hiyo nyie kwenu dhambi ni vita tu? kwanza hamuoni kuwa wazungu ndo wanafuata mali za waarabu ndo mana wanawatibulia amani ili waweze kuchota mafuta yao, na DRC wamevurugwa ili watu wachukue almasi, juzi juzi wametibua libya..apa bongo pia tukiwanyima nyima dhahabu na gesi hawakawii kuwapa zanzibar au chadema silaha tupigane wao waendelee kuchota mali..

suala la watu fulani kukosa maadili ya kidini huwezi kusema ni kutokana na dini yao...tukianza kuchambua nchi za kikristo apa zenye mambo ya ajabu hatutamaliza ntakusaidia kidogo kitu...

tafuta research data za europe kuhusu yafuatayo uone kwanini muslim community inaheshimika sana europe

google police reports on below issue..
- number of muslim drunk and drive cases
- number of muslim women abuse cases
- number of muslim neighborhood violence cases
- number of muslim rape cases
- number of muslim young age clubbing and alcohol abuse cases

hutokuta kijana wa kiislam Ulaya kafanya vituko vya ajabu ajabu sijui gays, sijui lesbians, etc
 
huyo anayewapandikizia viongozi ni nani ? na kwa faida gani?
 
Duh! we unaamini kabisa hayo makundi yana dalili ya kuteka dunia? na unaamini kabisa hao wakubwa wa dunia wamewashindwa?
Asante kwa kuniona.
Ninachosema ni swala la kiuchambuzi tu.
Kila kitu kilianza kwa wazo na matendo ya kiwango kidogo halafu kikakua.
Ninachouliza kama hawa wanaharakati wa Ki-Al-Shabab, Bokoharam nk.
Wanaitaka dunia ya aina gani ?
Ki darubini ya mbali kama watafanikiwa kuitawala dunia hapo baadae labda.
Wata zi chukulia vipi jamii mbalimbali za dunia na kuzihudumia ?





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kikwajuni Unaweza Kutofautisha Kati Ya Nchi Za Kidini Na Nchi Za Kidemocrasi
 
Kwani Population ya Muslims in Europe ni kubwa kuliko ya wazungu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…