R.I.P. Dr. Remmy Ongara

R.I.P. Dr. Remmy Ongara

Nakumbuka marehemu alizungushwa kwa miaka mingi sana ktk kupata uraia wa Tanzania,
siku aliyopata alifanya kasherehe ka kujipongeza.
 
... his songs, a University of life to keen listeners!!

Tangule Dr Remmy, tangulia tu, nenda kwa baba ukapumzike kwa amani ya milele!!!
 
kuna ule wimbo wake sijui unaitwaje ila nkumbuka mistari yake...

mwizi anakulikana... polisi wapo..... mahakama zipo... ya nini kuunda tume

kuna mtu ana hyo ngoma......?
 
Wote njia yetu moja..
Tu mavumbi na mavumbini tutarudi...Roho wa Mungu akupe pumziko la amani
 
R.I.P Remmy

Nitakukumbuka kwa nyimbo zako ambazo ni kama unabii unaotimia kwa wakati wake, uliona mbali.
 
dah!ndio nimesikia kwenye radio kama dakika tano zimepita hivi.kwani alikuwa anaumwa?
 
Wote njia yetu moja..
Tu mavumbi na mavumbini tutarudi...Roho wa Mungu akupe pumziko la amani
Roho wa Mungu ndo nani tena! Mwenyezi Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amin
 
RIP Dr Remmy,

Kwetu sisi tuliomwana akipanda hadi kilele cha mafanikio, hatutamsahau kamw huyu gwiji wa muziki. Ngoja nijaribu kukubuka baadhi ya nyimbo zake,

1. Narudi nyumbai...Ft Cosmas Chidumule
2. Amisa..mtoto wa kigogo
3. Mwanza makoroboi (sina hakika kama ndio title yake)
5. Kilio cha samaki
6. Ukijua kucheza (sina hakika kama ndio title)
7. Dole
8. Fadhili ni utumwa
9. Nalialia mwana
10. Penzi lawaua n.k .......

The guy was really talented...Nenda baba, kawasalimie wote waliotutangulia mbele za haki. Pia mshukuru sana Mungu kwani alikupa nafasi adimu ya kutubu dhambi zako ukiwa hapa duniani. Wengi huwa hawapewi hiyo nafasi..

Bwana alitoa, bwana ametwaa...!!
 
Inalilah wa inalilah rajhun! Katangulia nasi tutafuata
 
RIP Dr...............
angalau wewe udokta wako haukuwahi kuzua gumzo..............

Bwana alitoa............... na Bwana ametwaa,................. Jina la Bwana lihimidiwe.................
 
Kila nafsi yenye uhai itaonja mauti. Pumzika kwa Amani Dr. Remmy Ongala.
 
RIP DR Remmy mara ya mwisho akihojiwa akiwa wodini alisema akitoka atawatungia wimbo wauguzi na madr wa muhimbili kwa kushindwa kuhudumia wagonjwa vizuri , israeli akumsubiri atimize lengo lake.
 
R.I.P Remmy, pole sana Kalimagonga, mi niliipenda sana ile track yake ya "MAMBO MAMBO, KWA SOKSI".
 
ule usio na tiba wala chanjo


mbona mnapenda kuwasema watu vibaya......umempima remmy ukaambiwa alikuwa na ngoma .........wewe umepima??

kwa taarifa yenu tu ni kuwa remmy hakuwa na ngoma......hiili alishawahi kuwadhibiitishia watu miaka ya nyuma...alikuwa anasumbuliwa na kiharusi....na complications nyingine...

Ni kati ya wanamuziki ambao wametangaza nchi kimataifa na muziki wake hauchuji ....

YouTube - Remmy Ongala & Orchestra Super Matimila ~ Ndumila Kuwili

YouTube - Remmy Ongala - Mziki Asili Yake Wapi

mtetezi wa wanyonge !!
 
dah RIP DR REMMY. jana tu nilikuwa nasikiliza kibao chake cha MUME WANGU. the guy was very talented. vibao vyake km siku ya kufa, athumani, mwanangu celina mwanza ooh mwanzaa
 
Back
Top Bottom