Beno ni mwanauchumi aliyebobea katika medani za kimataifa. Baadhi ya wachangiaji walivyomuelezea hapo juu ni sahihi. Kwa kuongezea tu, huyu jamaa aliwahi kuwa mshauri wa Thabo mbeki katika nyanja za uchumi. Makabrasha yangu yanaonyesha kuwa Beno ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kwanza wa TRA board chini ya Ben mkapa.
Kama atabahatika kupata hiyo nafasi (dalili zinaonyesha hivyo), basi hana budi kucheza muziki kwa kufuata style ya mabosi wake--kikwete,lowasa, Meghji/rostam. Akicheza muziki tofauti na wenzake, atakuwa anajitafutia tiketi ya kwenda Boston kwa ajili ya matibabu.