Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
sasa mimi nikianza kuongelea upendeleo kwa watu wetu naambiwa kwamba "mbaguzi na mgumu kuelewa" tatizo kubwa na watanzania ni wagumu sana kuukubali ukweli tunaiangalia dunia vinginevyo kabisa utawaona akina mwakijiji na wenzake siku zote wakipiga domo kuwatetea wageni hapa kwetu mimi nimesema ni lazima tutoe upendeleo kwa watu wetu kwamba watu woote ambao hawana asili ya kwetu hata kama wamezaliwa hapa kwetu ni lazima tuwatofautishe na kuwanyima kwa makusudi kabisa haki sawa na sisi kwani ndivyo dunia ilivyo, kupingana na hilo ni kujaribu kuukataa ukweli ambao upo dhahiri, wewe mwenyewe umesema kwamba huko ulipo unabaguliwa na ukija hapa nyumbani pia unabaguliwa sasa swali linakuja Je ni mpaka lini tutaendelea kuwa watu wa kudharauriwa? Kumbukeni kwamba mwanadamu anaishi dunia kwa miaka mingi sana na mpaka leo hajweza kubadilisha huo ukweli wa upendeleo sasa nyie akina mwanakijiji ni kina nani mnaofikiri kwamba mna suluhisho la matatizo ya binadamu?
Narudia tena VITAMBULISHO TOFAUTI KWETU NA WATU WENYE ASILI YA NJE KWANI KILA KITU KINAANZIA HAPO BAADA YAPO TUNAKUJA SHULE, KAZI, MAKAZI, MAZISHI, USAFIRI n.k
sasa angalia yale yale unaukataa ukweli tena, hayo yoote unayoyasema yanasababishwa na kutokuwa na upendo wa kweli kwa nchi yetu na watu wetu, mapenzi ya kweli yanatokana na kuthamini watu wako, lugha yako, nchi yako kwanza na mengineyo yote ni daraja la pili sasa wewe kwa kuandika kiingereza wakati sisi sote hapa ni watz tayari unaonyesha mapungufu ktk fikra zako, sasa utawezaje kuanza kufikiria kukomesha rushwa kama unathamini wageni kuliko wenyeji????? watu kama ninyi na akina mwanakiji ni sarakani ktk nchi yetu!
Huu ni mfano tu wa matatizo mengi yanayoendelea kwenye hoteli hizi za kitalii hasa huko Zanzibar ambako mahoteli ya kitalii yanayomilikiwa na wa Italia.
Heshima mbele wakuu... ukweli ni kwamba hii mambo ya ubaguzi kwa sasa ni kila mahali.... nenda hata pale Mlimani city, kuna maduka ukiingia kuna walinzi wanakuwa aimed kukuangalia wewe.... sikatai kwamba kuna vibaka lakini kuna ways to control that than the way they are doing now sababu kwa kweli inatia aibu. kibaya zaidi watu wanaokuwa mstari wa mbele kutubagua ni waswahili wenzetu tena wanakuwa wakali kuliko hata mabosi wao.... SHAME ON THEM!!
``Since terrorists have no labels, the management decided to restrict an influx of local people into the lodge,`` the hotel boss noted.
Ningekuwa mimi nisingekubali: tungezipiga hadi niruhusiwe!
Mimi siamini kama kuna hoteli inayoweza kuwa na policy ya kuzuia watu weusi nchini Tanzania. Kuwa makini nao, ndiyo lakini kuwazuia hapana. Kuzuiwa mtu mmoja si lazima itokane na ubaguzi. Inabidi wazuiwe wengi zaidi ambao wana stahili ya kutumia hizo huduma ndiyo tuseme kuna ubaguzi.
Swali ambalo wengi tunalipiga chenga ni jee mwenye hoteli ana haki ya kuchagua nani ambae ataruhusiwa kupata huduma yake? Je, mwenye hoteli akisema kuwa huduma za baa zitatolewa kwa wale waliopanga vyumba na wanachama wa klabu yake napo ataonekana ni mbaguzi?
Najua vitendo hivi vinakera. Lakini wakati tunalalamika ni vyema tukiwageukia ndugu zetu na kuwaambia kuwa vitabia vyao vinatuharibia wengi! Hakuna mfanyabiashara atakaependa wateja wake watembee kwa hofu ya kushambuliwa au kuibiwa wakiwa katika eneo lake. Tembea na kamera yako waziwazi katika fukwe zetu saa za jioni halafu uone yatakayokupata! Hii haipaswi kuwa hivi. Kwetu wenyewe na hasa kwa wageni wetu.
Amandla....
Mkuu Fundi Mchundo, heshima mbele.
Labda sijakuelewa vizuri, unasema huamini kwamba kuna policy kama hiyo, mbona wenyewe wamekubali?
Two of its senior officials - Group Operations Manager Fred Tenga and General Manager Hamis Juma... saying ``Since terrorists have no labels, the management decided to restrict an influx of local people into the lodge,`` the hotel boss noted. A panicky Tenga apologized and said the policy was being withdrawn with immediate effect.
Na wamezuiwa wengi, kijumla jumla, sio mmoja. Sasa sijui kwa nini unasema "...inabidi wazuiwe wengi zaidi ambao wana stahili ya kutumia hizo huduma ndiyo tuseme kuna ubaguzi." Labda sijakuelewa kwa kweli.
Halafu kuhusu hilo "swali tunalolipiga chenga" la haki ya mmiliki kujiamulia wateja wawe wanachama au waliopanga vyumba, nadhani hilo swala ni muhimu sana lakini sidhani, Fundi Mchundo, kama linahusika hapa. Na hata hilo la wizi wa kamera za watalii, hilo nalo ni tatizo lakini tusilichanganye hapa kwa kuufinika baibui ubaguzi ambao mwenyewe umesema unakukera. Wengine tanaona ubaguzi sio unakera, la, unavunja sheria za nchi.
Kwa hiyo nadhani, Fundi Mchundo, hayo mengine sio kwamba tunayapiga chenga, hayapo uwanjani hayo. Huyu mmiliki hapa hakusema amekatalia mtu kwa sababu hakukodi kitanda pale, la, ni kwa ajili ya rangi yake, nukta.