Radi haipiti katika mawimbi ya simu (radio waves)

Radi haipiti katika mawimbi ya simu (radio waves)

Mwaka 2012 UDOM kuna mshikaji alikuwa anaongea na simu palikuwa na mvua,ilishuka radi ikapita naye
 
Hat transformers huwa zinabutuliwa na radi licha ya kufungwa lighting arrestors
 
Mimi natoka nje ya mada ila ni swali linalohusiana, kuna mtu aliniambia huu umeme una nguvu kuliko radi, kama upo karibu na radi inapiga sana bora usubiri hapo inaweza piga maeneo ya karibu lkn sio karibu na hii high tension power line.

View attachment 1707918
Aljkudanganya radi ndio umeme wenye power kuliko vyote ila ukikaa hapo radi itapiga izo nyaya ww huna cha kuhofia
 
Ndugu achana kabisa na kitu kinachoitwa Radi. nakumbuka kuna mwaka mazungu walifunga mtambo wa PBX (mtambo wa mawasiliano)kwenye halmashauri ya Morogoro.walifunga na vitu flani vinaitwa Arrester ili kuzuia Radi.Kuna siku ilipiga Radi ya hatari, ikaondoka na mtambo pamoja na Arrester zenyewe zilizokuwa zinazuia Radi.

Kifupi ni kwamba hakuna kifaa kinachokupa uwakika wa 100% kwenye kuzuia Radi
Ndege huwa zinazuiaje rad
 
Tuwekane sawa, ukiwa unatumia simu ya mkononi ndani mwako, na radi zinapiga nje, hata uweke 4g radi haidhuru simu. Radi haipiti katika mawimbi ya simu (radio waves). Radi ni umeme, hivyo husafiri sehemu zipitishazo umeme tu. Jiachie na internet ukiwa ndani ya nyumba yako, ila simu isiwe charging tu.
Ngoja ujidanganye, radi ni umeme na simu ni conductor wa electricity zoea tu kuna siku utakaushwa ndo ushangae
 
Mtoa mada hujui unachokisema aisee, hivi miti mirefu huwa ina umeme, pia naomba uniambie nini maana ya electromagetic wave
 
Mtoa mada hujui unachokisema aisee, hivi miti mirefu huwa ina umeme, pia naomba uniambie nini maana ya electromagetic wave
Kuna electro na magnet hapo...dogo wa form 4 alichomoa hili swali fresh.
Ni vibrations zinakua produced as a result of electric na magnetic fields zinapokutana
 
Hujakaa sehemu zenye radi kali, ungeelewa tu. Kuna mwaka fulani kuna dogo alibisha akawa anaongea na simu wakati wa kimvua mvua fulani, ikashuka ikapita nae na kujeruhi makumi waliokuwa jirani yake, radi sio ya mchezo mchezo.
 
Nimewahi kupigwa na shoti ya radi umbali wa kama mita 13 hivi mwaka 2002 hatari sana.
Yaani unawaka ule mwanga na moshi juu ndio wakati huo huo unapigwa shoti kwenye eneo moja la mwili halafu ndio unasikia ule muungurumo mkubwa.
 
radi ni umeme, kwa hiyo inapita kwenye njia za umeme, kama kuna radi nje vifaa vilivyoungwa kwenye umeme vitadhurika (radio, tv n.k) kwahiyo ni bora ukachomoa vifaa vya umeme kutoka kwenye switch mpaka ziishe
Kingine radi inaanza kupiga object ndefu zaidi kama ghorofa au mnara! Haiwezi kupiga object ya chini ikaacha ndefu
 
Niliendaga Iringa msibani halafu kijijini ndani ndani kwa siku 3

Sita kaa nije kusahau zile radi aisee
Sikuwahi kabisa kukutana experience kama ile kabla

Radi zilikua zinaunguruma utafikiri ndio mwisho wa dunia
Kuna jamaa alikua na T-shirts nyekundu aisee ilibidi aitupe kesho yake asubuhi [emoji23][emoji23][emoji120]

Hapo hakuna kuwasha simu kabisa na power bank tumeviacha kwenye gari sababu mjadala ulikua kama huu mnaojadili hapa
 
Mwaka 2012 UDOM kuna mshikaji alikuwa anaongea na simu palikuwa na mvua,ilishuka radi ikapita naye
Yes, nakumbuka alikuwa anatoka kula na washikaji ikamchambua yeye. Kesho yake tukaaga mwili na siku hiyo mademu wote walivaa kwa heshima hadi tukasema kumbe mademu wanajua jinsi ya kujistiri.
 
Acha kukaza ndoga hio. Fungua ubongo huo
Screenshot_20211114-104245_Chrome.jpg
 
Ndege ziko coated na kitu glan hivi nimesahau jina kuzuia radi
Radi haizuiliwi na chochote. Ikiamua kuharibu inaharibu tu. Niliwahi kuona clip moja, ndege ilipigwa na radi ikawaka juu kwa juu na kuteketea kabisa!!
 
Back
Top Bottom