Debby the FEMINIST
Member
- May 4, 2020
- 32
- 37
Mkazi wa kijiji cha Mpalu kata ya Nakahako Wilayani Newala Mkoani Mtwara Zuhura Swalehe Uheche Miaka( 35) Amefariki dunia baada ya kupingwa na Radi february 07 2021 wakiwa kwenye banda la biashara
Akielezea tukio hilo Diwani wa kata ya Nakahako Rashidi Lugomba amesema tukio hilo limetokea majira ya saa saba mchana ambapo Zuhura na wananchi wengine walikuwa wakitoka kuzika kijijini hapo na mvua ikanza kunyesha hivyo ikawalazimu kujistiri kwenye banda la biashara wakisubiri mvua iishe ndipo radi ikapiga na kuleta madhara kwa watu watatu
Aidha diwani huyo amewataja wengine waliojeruhiwa kuwa ni Amina Joseph (29) na Juma ahmad Mpadi (30) ambapo wote walifikishwa katika hospitali ya Wilaya Newala baada ya kutokea kwa tukio hilo
Mganga wa zamu hospital ya wilaya Newala Benedict Mkumulo amethibitisha kuwapokea Zuhura Swalehe na Juma Mpadi na wakafikishwa moja kwa moja katika chumba cha dharura na kuhudumiwa na muuguzi Simoni Siame ambapo vipimo vilionesha Zuhura Uheche tayari amepoteza maisha na kueleza kuwa Juma Ahmadi anaendelea na Matibabu mpaka sasa.