beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Wanafunzi watatu wa shule ya msingi Mkulima wamefariki dunia baada ya radi kupiga kwenye chumba cha darasa walichokuwa wanatumia.
Tukio hilo limetokea katika mji wa Nakuru nchini Kenya siku ya Ijumaa jioni wakati wa kipindi cha michezo Shuleni hapo.
Mbali na vifo vya watatu hao umedaiwa kuwa watoto wengine 53 wamejuluhiwa na wamepelekwa kwenye hospitali moja huko mjini Nakuru.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Thomas Sisa ameeleza kuwa watoto hao walikuwa wanarudi darasani kutoka kwenye mchezo wa mpira kwenye viwanja vya shule hiyo.