Baadhi ya watangazaji wa RFA hutangaza Star Tv pia. Kiswahili wanachotumia ni ovyo sana na si hilo neno la 'lakini ' tu, ila maneno mengi wanayatumia vibaya. Mojawapo ni 'kuweza'. Utasikia wanasema: 'Ndege ya ATCL iliweza kukwama kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza'
Pia si hayo maneno tu ila uchanganyaji wa herufu 'l' na 'r' kiasi cha kuharibu majina ya watu na vitu kama Elasto Mbwilo badala ya Erasto Mbwillo (Mkuu wa mkoa, Manyara) Saida Kalori badala ya Saida Karoli(Mwanamuziki wa nyimbo za jadi)au marelia badala ya malaria, roli badala ya lori nk.
Eti wamesomea uandishi wa habari! Uandishi wa habari bila lugha?Kichefuchefu kitupu!