Nimekuwa nikisikiliza kipindi cha RFA kinachozungumzia magazeti kila siku saa 12.30 asubuhi. Nimegundua watangazaji wanatumia neno lakini visivyo hasa kwa kuunganisha taarifa zisizofanana au kuhusiana. Nijuavyo mimi neno hilo hutumika kwa kutoa kasoro au kuunganisha habari zilizo sambamba. Isitoshe neno hilo linatumika saana au kurudiwa rudiwa mpaka inakera. Kituo hakina wasanifu wa lugha au ndio watangazaji makanjanja wasiojua lugha wameshawaingilia?