Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
TCRA imekituhumu kituo cha utangazaji cha RFA kukiuka kanuni na maadili ya utangazaji kupitia kipindi cha 'amka na BBC' kwa kurusha maudhui bila kuzingatia mizania ya habari walipokuwa wanamuhoji Makamu mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu juu ya viongozi wa chama hicho kutoshiriki kutoa heshima za mwisho kwenye msiba wa hayati Benjamin Mkapa.
TCRA imesema mtangazaji wa kipindi aliruhusu kurushwa habari iliyoegemea upande mmoja kwa Lissu kutoa tuhuma na kulalamika kuwa serikali ilimnyima nafasi ya kutoa heshima za mwisho bila kumtafuta msemaji wa serikali ili aweze kutolea ufafanuzi tuhuma hizo.
RFA wanatuhumiwa kukiuka kanuni Na. 15(2)(b) na (c) na 16 za mawasiliano ya kielektroniki na Posta(Maudhui ya Utangazaji na Televisheni) 2018.
Saa 5 asubuhi ya tarehe 10 Agosti, 2020 itakuwa ukomo kwa uongozi wa RFA kufika ofisi za makao makuu ya TCRA zilizopo Dar es Salaam kutoa utetezi wao katika shauri dhidi yao wa kimaandishi na kufika mbele ya kamati kujieleza kwanini kituo chao kisichukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka kanuni za huduma ya utangazaji.
SHERIA INASEMAJE?