Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Radio One Sterio mnapotusomea habari za rais wa Zanzibar haziwezi kuwa ni habari za kitaifa, hizo ni habari za taifa la Zanzibar lenye serikali yake na katiba yake.
Siku hizi kumezuka mtindo wa kuifanya serikali ya Zanzibar kuwa ni ya muungano! Na huu mtindo unafanywa na viongozi wa serikali ya muungano na kuifanya Zanzibar inaongozwa kwa pamoja na viongozi wa muungano, hii ni kinyume na katiba na wanafanya hivyo wakilenga uchaguzi mkuu. Kikatiba viongozi wa Zanzibar si viongozi wetu bara kwani hatujawachagua, hao ni wa wananchi wa Zanzibar na serikali yao ya Zanzibar, hivyo habari za serikali ya Zanzibar zitangazwe kuwa ni za Zanzibar na si za muungano.