Radio Safina: Mbinguni kuna spea za kizazi hivyo hata kama uliondolewa kizazi utazaa bila kizazi

Pia zipo spea ya meno, hata vibogoyo watalia na kusaga meno.
 
Kule jukwaa la dini sioni watu ....Habarrrrr njema kwa wenye matatizo ya vizazi, kwa mara yakwanza katika maisha yangu nilisikia jana kuwa kuna spea za kizazi..... INAWEZEKANA???


Kwa kweli Mi binafsi nina IMANI tosha kabisa.
Tunaposema "HAIWEZEKANI" MUNGU anasema "YOTE YANAWEZEKANA" Luka; 18;27

cc; Meljons Preta

Msibishane na wehu humu jamvini kwani ndiyo wale wale.

Hakuna linaloshindikana kwake Bwana wetu!
 
Last edited by a moderator:
Haya ndio madhara ya matumizi ya pombe aina ya viroba,mkiambiwa muache hamtaki, mimba mchokonoe wenyewe vizazi viharibike eti mungu awape spare.? Nina mashaka na huyo mungu kwakweli... Na kama ni ivyo duniani hakuna dhambi..

Aiseee kama huna cha kusema si ukae kimya????
Nyie ndo mnaopataga shida na kukimbilia kwa waganga wa kienyeji badala ya kuamini kwa Mungu hakuna lisilo wezekana,wenzenu tunaamini hivyo coz ukimwamini Mungu hakuna kigumu....
 
Duh hii habari nzito, ila inategemea na imani ya mtu


Mungu hashindwi na chochote lkn

Mbona keshashindwa na mengi tu? Mfano kuondoa dhambi na taabu duniani,ameshindwa kuifanya dunia iwe sehemu salama ya kuishi,ameshindwa kumdhibiti shetani,ameshindwa kuondoa njaa,magonjwa,umaskini,ubinafsi,ufisadi,uuaji,nk ametufanya tumkufuru ili atuchome moto!! Tafakari.
 
kufuru zote mtasamehewa, ila atakaye mkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.
 
endeleeni kutoa mimba kiholela au kutumia madawa ya uzazi kiholela mkitegemea mbinguni kuna spea za kizazi
Mungu ameshakuumba mkamilifu akakupa na uwezo wa kuzaa unajiharibu ukitegemea spea?
acheni imani za kitoto, Mungu hajaribiwi kwa namna hiyo.
Ni wale tu wagumba wa kuzaliwa hapo ndio panaweza kutokea miujiza lakini sio wa kutolewa kizazi
wachungaji wamewashika kweli kinamama wa Kiafrika na watu wenye ngozi nyeusi
 
...kama unaamini katika Mungu asiyeshindwa jambo lolote na aliye hai jana,leo na ata milele,kama unaamini uwepo wa Mungu huyo then hakuna cha kushangaa hapo,kama ameweza kuumba binadamu basi hatashindwa kuweka kizazi kwenye tumbo la mwanamke...
 
kuna vitu vngine ni kumkufuru mungu. Navyojua mimi ukiwa dunian kama huna uwezo wa kuzaa unaweza ukazaa kwa muujiza wa mungu imani yako itakuokoa. Ila huko mbinguni cdhani kama kuna kuzaa na hizo spea ndo kwa mara ya kwanza nasikia hilo
 
Capt Tamar, MUNGU (NIPO AMBAYE NIPO) wala hajashindwa maana yeye ni MUNGU wa kutimiza ahadi (COVENANT GOD), duniani ni himaya ya shetani aliyetupwa na MUNGU mwenyewe kwa kumkosea ndiyo maana hayo yote uliyoyaorodhesha yanafanyika duniani. Pia kumbuka MUNGU ni mwazilishi wa demokrasia, amekuwekea dhamira moyoni umchague YEYE au shetani.

Kwa hiyo kuwa fisadi, muuaji, mbinafsi ni chaguo la mtu kutoka moyoni mwake. MUNGU hajashindwa ila yale yaliyonenwa yanaachwa yatimie. Kama angeshindwa basi watu wote duniani tungekuwa tumeshakufa maana jukumu kuu la shetani ni kuangamiza.

Tena MUNGU aalivyokuwa wa huruma amekusikia ulichosema ila amekusamehe na unaendelea Kutumia jua lake, hewa yake na kuna siku utakiri MUNGU HAJASHINDWA.
 

yaah!kule yaeda chini ni manyara!kimsingi radio hii haiwakilishi imani bali ni wapuuzi wachache wanaojaribu kupotosha umma,kuna siku hii radio ilidanganya umma kuwa kuna mchawi kaombewa na kuangunga huko tengeru kumbe bibi wa watu alikuwa ni mgonjwa wa akili na chupuchupu wananchi wamuue!hii radio ni ya kipuuzi na kimburula...poleni kwa ukweli mchungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…