Radio stations za Kenya zipo mbali sana kiuchambuzi kuliko za Tanzania ambazo ni udaku tu

deblabant

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2022
Posts
2,650
Reaction score
4,065
Niko hapa mpaka wa kenya na Tanzania nasikiliza radio za kenya. Ki ukweli wako mbali sana katika uchambuzi wa masuaala mbalimbali ya siasa, uchumi na ya kijamii. Hakuna haja hata ya kujiunga na DW au BBC kusikikiza issues. Hizi hizi zinatosha.

Huku kwetu sasa ni mipira tu kuanzia asubuhi mpaka usiku wakitoka hapo eti ni mashamsham ya pwani. Kwa kweli sisi watanzani tumejaa umbumbumbu tu hakuna chochote tunachojua. Ikitokea tukawa wamoja kwenye shirikisho la afrika mashariki kila kitu basi tutaambulia patupu.
 
Kwa upande wa redio hapa kwetu tumepigwa pakubwa mno.Wachambuzi wa michezo kila saa.Kilimo ni uti wa mgongo hakuna mchambuzi hata mmoja,halafu ndio utawaambia vijana kilimo kinalipa au viwanda wakati hawajawahi kusikia.Kwa ujumla saa nyingine tunalaumu vijana ila sisi wahatibifu kupitia wanachosikia.
 
Niko hapa mpaka wa kenya na Tanzania nasikiliza radio za kenya. Ki ukweli wako mbali sana katika uchambuzi wa masuaala mbalimbali ya siasa, uchumi na ya kijamii. Hakuna haja hata ya kujiunga na dw au bbc kusikikiza issues. Hizi hizi zinatosha.

Huku kwetu sasa ni mipira tu kuanzia asubuhi mpaka usiku wakitoka hapo eti ni mashamsham ya pwani. Kwa kweli sisi watanzani tumejaa umbumbumbu tu hakuna chochote tunachojua. Ikitokea tukawa wamoja kwenye shirikisho la afrika mashariki kila kitu basi tutaambulia patupu.
Hizi za kwetu zinazomilikiwa na wapakwa mafuta ya Pdidy ziko kitoto sana
 
Wakenya wametuzidi mbaali sana katika mambo mengi.

Mara nyingi nikimis sana vibe huwa nina tune radio za kenya online nakula zangu reggae 🎶 za kutosha na taarifa za maana. (Bongo kila muda ni ma mipira tuuuu ushogaa ushooga mpaka yanaboa)

Yaani siku hizi naijua kenya kama nilishawahi kufika vile.
 
Sio kila linalofanyika Kenya ni lazima lifanyike Tanzania...msipende kuiga iga nyie Gen Z ..nyie haya tu!
 
Tanzania hamna kitu, Radio za Zambia tu hapo wapo vzr
 
Siyo kwamba watangazaji wa kwetu hawana uwezo wala weledi bali ni kila mtu anawaza hatma ya maisha na familia yake kwasababu uhuru wa vyombo vya habari kwa hapa nchni ni zero.

Kuna siku nilifuatilia mahojiano ya Rais wa Kenya William Ruto na waandishi wa habari. Aisee ni balaa Ruto anapigwa spana kweli kweli hapa kwetu mwandishi akiuliza maswali yale ameisha
 
Wana uhuru wa kutoa maoni hata vyombo vyao vya habari kwa kiasi kikubwa vipo huru. Huku kwetu Radio au TV ikitoa habari ambayo ipo tofauti na watawala chombo hicho kinafungiwa, sasa kwanini wasijikite kwenye uchambuzi wa soka asubuh mpaka jioni?
 
Soko la redio ni soko huru hivyo bas m2 yoyote ana uhuru wa kuweka maudhui yoyote ingali hayapishani na sheria,taratibu na kanuni za nchi.

Tukirudi kweny maada yako jukwani ni dhahiri shairi unachokisema na hii imetokana na jamii yetu kwa ujumla. Aghalabu kwa mtu kuweka mada ambayo sio pendwa kutokana na ukweli kwamba wamiliki wa radio nao wanataka faida.

Jamii yetu ikibadilika nakubakikishia vipind vitakua vingi vya maana kutokana redio hufuata uhitaji wa walaji.

Mwisho, kutokana na uhuru wa soko ni vyema hata wewe pia unaweza fungua redio ukaweka contents zako.
 
Niko hapa mpaka wa kenya na Tanzania nasikiliza radio za kenya. Ki ukweli wako mbali sana katika uchambuzi wa masuaala mbalimbali ya siasa, uchumi na ya kijamii. Hakuna haja hata ya kujiunga na DW au BBC kusikikiza issues. Hizi hizi zinatosha.

Huku kwetu sasa ni mipira tu kuanzia asubuhi mpaka usiku wakitoka hapo eti ni mashamsham ya pwani. Kwa kweli sisi watanzani tumejaa umbumbumbu tu hakuna chochote tunachojua. Ikitokea tukawa wamoja kwenye shirikisho la afrika mashariki kila kitu basi tutaambulia patupu.
Mfumo qetu ndiyo unataka hivyo

Ova
 
Tanzania hakuna vyombo vya habari bali kuna wapambe wa Samia na CCM! Vinafadhiliwa kila kitu na Samia na kila taarifa vinapotoa lazima vimtaje Samia na visipofanya hivyo kuna hatari vikafa kwa kukosa ufadhili au kufungiwa!

Kuna kila sababu ya kubadilisha sheria ya vyombo vya habari ili vipate uhuru kamili!
 
Niko hapa mpaka wa kenya na Tanzania nasikiliza radio za kenya. Ki ukweli wako mbali sana katika uchambuzi wa masuaala mbalimbali ya siasa, uchumi na ya kijamii. Hakuna haja hata ya kujiunga na DW au BBC kusikikiza issues. Hizi hizi zinatosha.

Huku kwetu sasa ni mipira tu kuanzia asubuhi mpaka usiku wakitoka hapo eti ni mashamsham ya pwani. Kwa kweli sisi watanzani tumejaa umbumbumbu tu hakuna chochote tunachojua. Ikitokea tukawa wamoja kwenye shirikisho la afrika mashariki kila kitu basi tutaambulia patupu.
Ushauri wako, tufanyeje sasa mkuu?
 
Sio kila linalofanyika Kenya ni lazima lifanyike Tanzania...msipende kuiga iga nyie Gen Z ..nyie haya tu!
Siyo kuiga bali uhuru kamili wa vyombo vya habari unatakiwa!
 
Niko hapa mpaka wa kenya na Tanzania nasikiliza radio za kenya. Ki ukweli wako mbali sana katika uchambuzi wa masuaala mbalimbali ya siasa, uchumi na ya kijamii. Hakuna haja hata ya kujiunga na DW au BBC kusikikiza issues. Hizi hizi zinatosha.

Huku kwetu sasa ni mipira tu kuanzia asubuhi mpaka usiku wakitoka hapo eti ni mashamsham ya pwani. Kwa kweli sisi watanzani tumejaa umbumbumbu tu hakuna chochote tunachojua. Ikitokea tukawa wamoja kwenye shirikisho la afrika mashariki kila kitu basi tutaambulia patupu.
Mimki siwezi kucomment ila naungana na wewe. Cha muhimu ni kujiuliza tumefikaje hapa, tumefikaje kwenye mkwamo wa namna hii, je ni elimu yetu|? je ni tamaduni zetu? je ni ujinga wetu? . Kuna andiko niliandika kipindi fulani ingawa halikuchangiwa na mtu hata mmoja, na hapo ndipo nikagundua kumbe inabidi kuandika mambo marahisi, sisi hatupendi nondo ngumu zenye kufikilisha.

"System can dictate/change the direction of thinking and behavior of people they are leading in order to allign with their needs to continue leading or avoid opposite opinions/challenges/threat"

Hiyo sentensi ndiyo bottom line ya utofauti wa ulichokiona. No further comments, we are the victims of our own system, we have reached a stage were we have no way out than dancing to the tone , the system, dictate us to dance.
 
Back
Top Bottom