Abel Lusinde
Member
- May 3, 2016
- 33
- 29
RAFIKI ANAYEWEZA KUWA ADUI WA ELIMU YA MTOTO WAKO
Utangulizi
Teknolojia ni nini?
Teknolojia ni matumizi ya maarifa ya kisayansi kwa malengo ya vitendo ya maisha ya mwanadamu au, kama inavyosemwa wakati mwingine, kwa mabadiliko na uendeshaji wa mazingira ya mwanadamu. (Encyclopædia Britannica)
Matumizi haya ya maarifa ya kisayansi, kama sote tunavyoweza kufahamu, yana faida lukuki na tena kutegemea na nyanja unayoizungumzia kama vile elimu, afya, kilimo, viwanda na kadhalika. Na maarifa haya ya kisayansi yanasaidiwa na vifaa vya kiteknolojia vyevye kubeba uwezo wa kuitikia amri ya mtumiaji kuhusu nini (maarifa hata ujuzi) kifaa hicho kimpatie yule anayekitumia, kama apendavyo mtu huyo. Vifaa nitakavyovijadili ni simu janja (ama ya kawaida) pamoja tarakilishi (computer) kwa aina zake ikiwemo tarakilishi mpakato (laptop) hata katika faida na madhara ya matumizi katika elime ya msingi na sekondari angalau kwa ufupi.
Hivyo tujikite kwenye elimu, hasa ya msingi na sekondari hapa nchini Tanzania, na hasa jinsi teknolojia haya Matumizi ya simu janja pamoja na tarakilishi zinavyoweza kuwasaidia ama kuwapoteza wanafunzi wa ngazi hizo, yaani faida na hasara ya matumizi ya vifaa hivi kupatia maarifa hasa katika mazingira ya nchi yetu.
Faida :
Kwanza, kutumia vifaa hivi vya kiteknolojia katika kujifunzia kwaweza kuwavutia wanafunzi katika kujifunza na kutafuta taarifa na maarifa zaidi katika mada fulani fulani. Aidha pamoja na kumrahisishia mwalimu kuwasilisha mada, pia kwa mwanafunzi anaweza kuvutwa zaidi kwa sababu ya namna anavyoshiriki moja kwa moja katika matumizi ama katika kuona mada kwa uhalisia zaidi, mfano picha na video.
Leo si jambo la kushangaza sana kuona watoto wengi wa umri wa kwenda shule na wale walio shule tayari kuwa wanavifahamu na hata baadhi kujua kuvitumia vifaa hivi vya kiteknolojia. Na huwa na furaha kubwa wanapofundishiwa au kuruhusiwa kuvitumia vifaa hivyo. Kwa hiyo, teknolojia hizo pamoja na kuwasaidia kuvutwa kwa umakini darasani, pia huwachangamsha na kuwasisimua zaidi katika kujifunza kwao.
Pili, kuwaandaa wanafunzi kwa wakati ujao wa ulimwengu huu wa teknolojia. Dunia yetu, kila kukicha, unazidi kuitegemea teknolojia, hivyo kuwa na uelewa mzuri wa vifaa hivi vya kiteknolojia na ujuzi sahihi wa kuvitumia katika elimu ya watoto ni muhimu ili kuwaandaa na kuwatayarisha wanafunzi kwa mafanikio yao katika elimu ya msingi na sekondari na baada ya hapo matumizi maishani. Kwa sababu hii si vibaya na si mapema kama tuzaniavyo mara nyingi, kwa watoto wa shule ya msingi au sekondari kuwaruhusu kuanza kutumia na kama matokeo kujijengea maarifa na ujuzi utokanao na teknolojia katika elimu yao kwa kutumia vifaa hivi.
Tatu, teknolojia huchochea kujifunza yeye mwenyewe na kwa wakati anapohitaji.
Kuwapatia na kuwaruhusu kuvitumia vifaa hivi vya kiteknolojia, angalau chini ya uangalizi kunaweza kuwasaidia wanafunzi hawa watoto kujifunza na kuchunguza mda wanazofurahia katika masomo. Tofauti na kizazi chetu cha zamani ambapo hata simu za kawaida hazikua rahisi kupatikana isipokua kwa wachache ambao walikua na uwezo wa kufanya hivyo, sasa, wanafunzi wanao ulimwengu wa taarifa na habari papo hapo karibu sana nao. Vinapotumiwa kwa usahihi na ipasavyo, vifaa hivi na teknolojia inayoviongoza vinaweza kuongeza mara dufu kujifunza ndani na nje ya darasa hata kuwapatia wanafunzi ujuzi na kuwawezesha kutafiti mada zinazowavutia kulingana na ngazi zao katika elimu. Mada hizo zinakuwa za kuvutia Zaidi zinapofafanuliwa kwa picha ama video.
Pamoja na kuangazia faida hizi chache tu, watoto wanapaswa kuelekezwa namna bora na sahihi ya matumizi ya vifaa hivi, wakitahadharishwa kuepuka matumizi yasiyo sahihi hasa yale ambayo hayana faida katika kujifunza kwao. Wafundishwe uhuru wa kutumia vifaa hivi lakini uhuru huo uwe na mipaka, maana uhuru usio na mipaka ni utumwa ulioziba macho ya mtumwa asione.
Hata hivyo kama wazee wetu wa zamani (wahenga) walivyosema, hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, hakuna zuri lisilokua na kasoro. Pamoja na teknolojia kuwa na mazuri mengi lakini isipotumiwa kiusahihi bila kuzingatia ‘miiko’ ya kiteknolojia na kijamii teknolojia nzuri hugeuka kuwa kitu kibaya sana chenye kuwapotosha, kuwaharibu na hata kuua malengo ya kielimu ya wanafunzi. Tuangalie madhara ama athari-changamoto chache pia katika matumizi ya vifaa hivi vya kiteknolojia.
Athari
Moja, uraibu wa kimtandao. Mara nyingi mtumiaji wa vifaa hivi asipokua makini, na hasa kama haweki tahadhari ama hakutahadharishwa juu ya uwezekano wa kuingia katika tatizo hili, hujikuta polepole lakini kwa hakika akishikwa na kung’ang’aniwa na uraibu (addiction) huu. Mraibu huwa tegemezi kwenye mtandao bila kuwa na uwezo madhubuti binafsi kujizuia na hivyo kujikuta akitawaliwa na kuendeshwa asivyotaka. Kukicha ni kukodolea macho kwenye simu ama tarakilishi hadi jua lizame bila kufanya kile chenye matokeo chanya. Tabia hii mbaya inaingilia na kuleta mfadhaiko ya mwanafunzi ama mtumiaji na kuathiri maisha yake ya shule, na yale ya nje ya shule. Tatizo hili laweza kutibiwa na wataalam wa afya ya akili, lakini kinga ni bora kuliko tiba.
Vilevile, matumizi ya vifaa hivi yanaweza kuharibu usikivu wa wanafunzi, hasa kama mwanafunzi ambae hakufundishwa na kupewa mipaka ya kimaudhui katika vifaa hivi vya kiteknolojia. Simu janja na tarakilishi zaweza kuwafikishia wanafunzi hawa wadogo maudhui ambayo hayafai ikiwa hakutakuwa na vizuizi ama kuchujwa kwa maudhui hayo kulingana na umri wa mtumiaji. Katika baadhi ya nchi zilizoendelea hili hufanyika kwa kuzuia kabisa maudhui flani yasipatikane kwa umri fulani wa watoto, hata kama wakiachwa wao pekeyao kutumia vifaa hivi.
Si ajabu ukakuta mtoto wa msingi au sekondari amezoelea kuangalia picha chafu, video chafu n hata kuiga kuyafanya anayoyaona humo. Matokeo yake ni nini? Ni kumpoteza kabisa mtto huyu katika misingi ya maadili ya kitanzania. Kwa ufupi, maudhui hayo yasiyofaa yakifanikiwa kumfikia mtoto, humomonyoa maadili na kuathiri utendaji katika masomo na maisha nje ya darasa.
Pia, teknolojia inaweza kuua ama kupunguza ubunifu kama wanaohusika wasipokua makini katika kuwasimamia watoto. Kwa sababu karibia kila kitu anachotaka mwanafunzi, hata utatuzi wa changamoto pamoja na kazi anazopewa darasani mtoto anaweza kuzitatua kwa kutumia vifaa hivi. Hali hii inaweza kupelekea mtoto, hata sipofika kwenye uraibu, kupunguza uwezo wake wa ndani wa kutatua changamoto, kufanya kazi za darasani na kuufikirisha ubongo wake ipasavyo kwa sababo kipo kisaidizi kinachoweza kufanya kazi zote hizo bila yeye ‘kusumbuka’. Hii inaweza kuwa hatari zaidi ya tunavoweza kufikiri
Hitimisho na Ushauri:
Wasimamizi na wadau wa elimu sote tunapaswa kuwa makini katika kusimamia elimu ya watoto hawa na hasa pale tunapoona umuhimu wa wao kuvitumia vifaa hivi katika kujifunzia ili wasije wakatoka katika malengo ya kuvitumia; hata inapobidi kumrudi mtoto unapogundua kuwa ametoka kwenye mstari wa matumizi yanayofaa ili kumrejesha kwenye lengo. Wala tusiwazuie kabisa kwa sababu kwa kufanya hivyo tunawazuia kupata faida ambazo baadhi tu nimezieleza hapo juu.
Kumbuka! Teknolojia ni nzuri na inafaa sana hata katika ulimwengu wa sasa lakini tapaswa kuwa na tahadhari kuwalinda watoto wetu na matumizi yasiyo na mipaka na yanayowavunjia maadili. Teknolojia yaweza kuwa baraka ama laana, inaweza kujenga ama kubomoa, sharti itumiwe kwa malengo mazuri na mipaka iliyo wazi itajenga kizazi kilicho imara na bobezi katika teknolojia hasa katika nyanja hii iliyojadiliwa hapa.
Asanteni.
Utangulizi
Mada hii inaangazia teknolojia na matumizi ya vifaa vya kielekroniki vinavyoweza kutumiwa na wanafunzi ama kufundishiwa au kujifunzia wao wenyewe. Teknolojia inazidi kuhitajika na kutumiwa angalau katika baadhi ya ngazi za kielimu na shule za kisasa hata katika nchi yetu. Lakini kwa baadhi ya wadau wa elimu, wazazi na walezi au wasimamizi wa elimu ya wanafuzni hasa wale wa shule ya msingi na sekondari wanapata ‘ukakasi” katika kuchukuliana na jambo hili.

Attachments
Upvote
0