Rafiki/ Ndugu zenu wanajua Kazi/ Biashara mnazozifanya?

Rafiki/ Ndugu zenu wanajua Kazi/ Biashara mnazozifanya?

BM X6

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2020
Posts
1,376
Reaction score
4,222
Jana nilishinda nyumbani siku nzima, sikuwa kazi nilijipea off, Sasa kabla siku haijaisha alikuja beshte yangu katika story nikamuelezea Biashara ambazo nataka kufanya ili anishauri.

Alinipa Ushauri wa kutosha lakini ushauri mkubwa aliyoniambia ni huu[emoji1484] nanukuu "Unajua kuna Baraka nyingi sana katika kufanya mambo yako kimya kimya, Midomo ya watu ila laana nyingi sana pale wanapo gundua jambo lako"

Baada ya kunambia hivyo nilitafakari sana na nikahisi tayari nishaharibu kila kitu kwasababu kama aliyoniambia ni kweli basi hata yeye nilitakiwa nisimshirikishe katika hili, nina uhakika gani kama Mdomo wake hauna Laana, halafu issue yenyewe ni Biashara na Biashara inataka matangazo hapa mtu unatokaje kwa ushauri huo hapo juu

Mnaofanya Kazi au Biashara ebu tuambieni watu wenu wa karibu hawajui Kazi/Biashara zenu mnazozifanya? Na kama wanajua unahisi Wana Athari yoyote katika kile unachokifanya?
 
Biashara ni marangazo ndiyo ila sasa itangazwe kwa wateja si ndugu wala rafiki wala jamaa ambao hata mia hawawezi changia ikidolola kwanini.

Ndugu, ulimwengu wa leo mwenye kupenda mafanikio ya kweli ni wazazi wako tu ila hawa sijui shangazi , sijui mjomba , sijui binamu ni wanafiki watupu.

Hawana wanachojari zaidi ya wivu pale mambo yakinyooka ila yakienda kombo pia kwao ni furaha sana ...

Ushauri tu

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
I got you bro[emoji1545]
 
Back
Top Bottom