Rafiki niliyemuamini akanipora mchumba, Mungu akanilipia!

Rafiki niliyemuamini akanipora mchumba, Mungu akanilipia!

Kisa kizuri mno! mno jamani!

Kinasikitisha....ila kuna mengi ya kujifunza.

Nakikopi na kukipaste kwenye word doc then nakiprint..

Ntakiweka kwenye arcive ya mavitabu yangu...







.....


Mpe pole sana mdada huyo..

Ila kama anataka mbegu tu....sio mbaya tukawasiliana but (vigezo na masharti kuzingatiwa)

..
 
Mkuu pole sana kwa mkasa uliokukuta,
Ila mkuu Mungu Hajakulipia kwa sababu angelikua analipa hata wewe usingelikua unaishi sasa hivi
 
Story ni nzuri na ina fundisha. Ila siku nyingine ujaribu kufupisha
 
Duh.. sad story, usikate tamaa mungu yupo pamaoja nawe utapata mwanaume wa maisha yako
 
Imenihuzunisha sana hii, lakin ni mambo ya kweli yanatokea ktk dunia hii, ndo mana cpendi na ctaki kuwa na marafiki an Im happy with my life!
 
eeeh, maskini!!!
Yani kama za Mtambuzi....na zaidi!
 
mungu amsaidie huyo dada apate mume nae siku moja apatwe kuitwa mama pia nampa pole sana kwa yaliyomkuta
 
Asante dada kwa stori iliyojaa mafundisho. Mungu anajua namna ya kuepusha watu wake kwenye matatizo na ulaghai wa sisi binadamu. Kuna vijana hapa mtaani kwangu ntawapa hii stori waisome iwasaidie.
 
Ni ushuhuda mzuri ambao unaelimisha. Shukrani kwako vukani uliyetuletea mkasa huu..........
Niliwahi kuuliza swali hapa JF kuhusu wanawake wanaowasaliti mashoga zao, BADILI TABIA alitoa maoni mazuri ambayo yalinivutia, naomba niyaweke hapa kwani yanafikirisha.

Uzi wenyewe ni huu hapa chini:

https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/192934-kwa-nini-wanawake-husalitiwa-na-mashoga-zao-kirahisi.html#post2824080

Na BADILI TABIA akasema hivi:

nadhani kuna sababu nyingi, baadhi ni:-
1. tamaa shoga, haswa pale anaposimuliwa mambo ya yule mwanaume lets say unamwambia shoga yako "bwana wangu mjuzi ananipeleka ananifanya hivi au vile" au pale shosti anapoona bwana wa mwenzie anamjali anampa hiki au kile simu mara kwa mara; anadhani akiingia na yeye atapata, au kama mwanaume ana fedha shosti anaweza kumtokea akijua atapata fedha nk

2. tabia mbaya ya mwanaume; kuna mijanaume mizinzi inatongoza hadi ndugu zako wa damu sembuse rafiki. na ukikuta na shosti ana tabia mbaya ndo inakua balaa

3. baadhi ya mashosti wanafanya hivyo kukomoa "tuone anachoringia kwa huyo mwanaume wake" au " naweza kumchukua huyo mwanaume wakati wowote"

4. wengine labda wana matatizo kisaikolojia jamani, kuna mdada yeye ni kujirahisi kwa waume wa wenzie, akimpata anafanya kama competition fulani, akiweza kupata attention ya mume wa mwenzie ndo anapata faraja. Sijui huu ni ugonjwa au vipi, ilifikia kipindi wanawake walipomshtukia wakawa wanamkwepa

wanawake wanatakiwa kuwa makini sana na hawa mashosti, usiache rafiki kumzoea mumeo/boyfriend. lazima kuwe na limit ya uhusianao kati ya rafiki na mume/boyfriend. haiwezekani kila rafiki akawa na namba ya simu ya mumeo, na ampigie anavyojisikia. akitaka kitu kwako badala ya kukupigia wewe yeye anampigia mumeo.
Hili pia linaenda hata kwa wanaume, asimzoee sana shemeji yake.

pia mwanaume makini aliyependa kwa dhati, anayemuheshimu mwenza wake hawezi kutembea na shosti wa bibi yake, kama kutoka atacheza mbali
 
Story ni nzuri na ina fundisha. Ila siku nyingine ujaribu kufupisha
Rutta, acha uvivu wa kusoma, mbona umeisoma yote?
Tukisema kuwa ni stori tutakuwa tunakosea, huo ni ushuhuda.
Hata hivyo naamini Mungu hajamlipia dada yetu ila ni makosa tu ya kibinadamu upande wa hao wanandoa na wala haikua kosa kuachwa kwa kuwa hakuwa mumewe.
Ntaamini Mungu kamlipia akipata mume toka kwa BWANA.
Wadada msipende kujirahisisha, mtaishia 'kupitiwa' na wachumba 50. Baneni chupi zenu.
 
mi ni mvivu wa kusoma lakini hii leo imenibamba.......dah......maswahibu mengine bana........
 
Back
Top Bottom