Rafiki wa Davido afariki akijaribu kuongeza uume

Rafiki wa Davido afariki akijaribu kuongeza uume

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Mfanyabiashara raia wa Uingereza na Nigeria, pamoja na influencer wa mitandao ya kijamii ambaye pia ni rafiki wa Davido, Igho Tiny Ubiribo, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 43 baada ya kufanyiwa utaratibu wa kuongeza ukubwa wa uume akiwa nchini Thailand.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na TMZ, Ubiribo, ambaye pia alikuwa akifahamika kwa majina ya Denisi au Ego, alifanyiwa utaratibu huo katika kliniki moja jijini Bangkok, ambapo madaktari walitumia mililita 40 za mchanganyiko wa hyaluronic acid na lidocaine.

Baada ya kufanyiwa utaratibu huo, Ubiribo alikwenda kupata massage akiwa pamoja na mke wake, Danielle Simba Allen.

Hata hivyo, akiwa katika shughuli hiyo alianza kupata maumivu makali ya kifua na baadaye alizimia mara mbili.

Alikimbizwa katika Hospitali ya Sukhumvit, ambako madaktari walifanya zoezi la kumrejesha katika hali ya kawaida (CPR) kwa zaidi ya dakika 100. Pamoja na juhudi hizo, Ubiribo alitangazwa kuwa amefariki dunia.


Taarifa za kitabibu zinaeleza kuwa chanzo cha kifo chake kilikuwa pulmonary embolism, hali inayotokea pale ambapo donge la damu linapoziba mshipa wa damu unaoelekea kwenye mapafu.

Kifo hicho kimetokea wakati Ubiribo akiwa likizo nchini Thailand pamoja na mke wake.

1788673118877.png



IMG_5724.jpeg
 
Influencer wa kinaija bana
Wana mambo mengi !

Ova
 
Alitaka kushindana na nini.

Anadhani ile sehemu inahitaji mashindano 😂
 
wanawake tuishi nao kwa akili

wanaume tunakufa kwa mambo mengi sana. lakini kina cha satistifactory ni nchi mbili tu wakuu yote ya nn haya ona sasa!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom