Rafiki yangu akifanya tiba za kienyeji hafanikiwi huku wengine wakifanikiwa kwa haohao wataalam

Mi nikienda kanisani mambo yanazidi kua magumu wenzangu wakienda vitu vinanyooka.

Nitaenda kwa waganga wanne kama case study na kurudisha majibu.
Umekaribia kutoboa,usiondoke kanisani utaharibikiwa.
 
Wanadamu tunatofautiana sana kiroho hata kama ni watoto wa mama na baba mmoja.

Kifupi tu ni kwamba huyo ndugu yupo katika himaya ya juu zaidi ya ile ya uchawi wa pembe, matunguri, kitabu na hata majini!

Ni mtengwa wa Bwana na hata huo uchawi hauna pa kujishika kwake hivyo hauingii katika systems zake. Hivyo kwa waganga hakutamsaidia ila atakwenda tu kama mapito ila ana njia zake nyingine za kufanikiwa.

Niliwahi ā€œkupelekwaā€ kwa mganga nilipofika akaanza kupabdisha mizimu yake tena kwa taabu. Ile mizimu ikasema umekuja kufanya nini hapa wewe? Umekuja kutujaribu sio? Hukukuwa na kitu cha maana na niliondoka. Baadaye Nilifikiri na nilijua kweli hiyo haikuwa njia yangu wala baba na mama yangu hawakuwahi kufanya hivyo kwani walinilea katika misingi imara ya Kikristo.

Huyo bwana kwa waganga sio pake yeye ni mtu wa juu kiroho na atafanikiwa kupitia njia za Aliye Juu (Mwenyezi) na mambo yake ni makubwa.

Haitakuwa rahisi, atapigana vita ya kiroho lakini atashinda na kama atapata mwalimu sahihi wa kiroho atafika viwango vya juu mno na kuwasaidia wengine wengi.

Hivyo anapaswa kuanza safari ya kumtafuta, kumjua na kumfuata Yesu Kristo ndipo maisha na usalama wake vilipo.

Na Mimi ninayo hii shida

Pole MKUU..... Huenda sio njia sahihi kwako jaribu kutafuta alternative ( upande WA pili)

Huyo ni kipenzi cha Mungu, Mungu hataki kumpeleka motoni Kwa dhambi ya shirki.....
Dawa aamke kila siku saa Tisa usiku, Kwa Imani yake aongee na Mola wake....pia atoe sadaka ya Siri.

Mkuu si useme tu ni wewe shida iko wapi! ukiona upande huo haufanikiwi mlilie Mungu hakuna kinachoshindikana kwake.


Mi nikienda kanisani mambo yanazidi kua magumu wenzangu wakienda vitu vinanyooka.

Nitaenda kwa waganga wanne kama case study na kurudisha majibu.

 
kwani ukisema ni wewe huyo unayetaka tiba utapungukiwa na nini.
Haya subiri wajuzi wa izo mambo
 
Destiny is all.
Ishi kawaida furahia maisha .
 
Hii itakua kweli
Nilikusoma sehemu flani, nachoweza kukusahauri punguza Sonona, furahia na shukuru baraka zako....shukuru Kwa afya, shukuru huna ulemavu, shukuru umesoma una vyeti......kwenye maombi shukuru zaidi badala ya kulalamika

Kisha anza kujipenda, jipende oga, jisugue, pendeza....watu wanaheshimu watu wanaopendeza.....pia kupendeza inaleta kujiamini na inafanya roho yako irelax.

unahitaji watu, jitoe out ukutane na watu....nenda sehemu ambazo utakutana na watu unaotamani kuonana nao, be charming ( Usiwe chupi mkononi)

Mwisho anza kumanifest mafanikio, assume umepata Kazi, assume namna utavyoutumia mshahara wako wa Kwanza.....vuta picha, vuta Ile furaha utayokuwa nayo na utabasamu as if umeshafanikiwa....

Fanya hayo, utanisimulia.
 
Sawa
 
Huyo kama mimi... Mpaka nimeamua kubaki kwa Mungu aliye hai tu...nilisimama vyema kwenye imani nafanikiwa
 
Mkuu mpe pole zake huyo rafiki yako mwambie anitafute mimi Herbalist Doctor MziziMkavu nipate kumtibia ili aweze kufunguka nyota yake na vifungo mikosi majini mahaba wote wapate kumtoka mambo yake ya maisha yaende vizuri. Mpe salaam zangu.
 
Mwambie aanze kuwachaji wale anaowaelekeza huko. Labda mafanikio yake yapo hapo na yy hayaoni
 
Kaka habari yako, mimi nina tatizo mdomo(lips) zinakauka sana na kutoa magamba mdomo umekuwa mwekundu sana ,tatizo lina muda wa miaka 8 na halijawahi kuisha nimejaribu dawa za kila aina za hospitali hadi kwa ma specialist wa ngozi sijapona ,naomba unisaidie tatizo langu hata kama kuna dawa za mitishamba , tatizo linanitesa sana ,naomba msaada wako maana una ujuzi wa tiba za asili ,huenda nikapona
 
Njooni pm Leo natoa namba Ila tafadhari mkiulizwa namba mmetoa wapi semeni uongo mnaoufahamu nyinyi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…