Rafiki yangu alipofariki nilitambua maisha ni mafupi kuliko tunavyofikiri

Rafiki yangu alipofariki nilitambua maisha ni mafupi kuliko tunavyofikiri

Sun is Sun

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2024
Posts
1,254
Reaction score
2,014
Habari zenu, hii iliniuma.

Nilipomuona rafiki yangu akiwa amelala ndani ya jeneza nilitambua jambo moja, maisha ni mafupi kuliko tunavyofikiri.

Mtu ambaye jana alikuwa anatembea, akicheka, akizungumza na kupanga kesho yake, leo amelala kimya. Hawezi kuamka tena, hawezi kusema neno, wala kuchagua anakotaka kwenda. Popote atakapopelekwa, anaenda tu, akiwa kimya kama sanamu. 😭

Cha kusikitisha zaidi ni kwamba hata aliyefariki leo aliamini bado ana muda wa kuishi. Huenda alikuwa na mipango ya kesho, ndoto za kutimiza na mambo aliyotarajia kuyafanya siku zijazo, Lakini leo hayupo tena.

Na sisi tulio hai, tuna uhakika gani kwamba tuna muda mwingi mbele yetu? Huenda kesho, mwezi ujao au miaka mingi ijayo, lakini hakuna anayejua zamu yake itafika lini.

Hapo ndipo ninapojiuliza, hivi sisi binadamu tunajivunia nini hasa? Tunagombana, tunachukiana, tunadharauliana na tunajiona bora kuliko wengine, kana kwamba tutaishi duniani milele.

Mali, umaarufu, uzuri na majivuno yote yana mwisho wake.
Tusijione special sana duniani. Sisi ni wasafiri tu, na hakuna anayejua mwisho wa safari yake.
Tupendane, tusameheane na tuwathamini watu tulionao kabla hawajawa kumbukumbu.

Tusisubiri mtu aondoke duniani ndipo tutambue thamani yake.
💔 Kifo kimetukumbusha kwamba tunaweza kupanga maisha yetu yote, lakini hatuna uhakika hata na kesho yetu.

Pumzika kwa amani, rafiki yangu. Kifo chako kimenifanya nitafakari upya maana ya maisha. Sasa ninaelewa zaidi kwamba sisi sote ni wageni katika dunia hii, na siku moja wote tutazima kama mshumaa.
 
Mpaka umri niliofikia huu aisee niliowajua na walifariki ni wengi mno...nadhani hii inanipa kukichukulia kifo kawaida siku kikigonga mlango...ila inaumiza kujua kwa zaidi ya asilimia 80 uwa kinakutoa roho kikauzu sana. Rafiki yetu ni mmoja ya walioungua kwenye ajali ya majuzi ya bus
 
Binadamu ni mwepesi sana kusahau,

Baada ya muda utamsahau huyo rafiki yako na hutakiwaza sana kifo kisha utarudi tu kwenye maisha yako ya kawaida,
Hiyo hali humtokea kila mtu anapofiwa na mtu wake wa karibu,
Maisha yataendelea tu kama kawaida baada ya muda.
 
Pole sana ndugu Sun is Sun kwa msiba wa rafiki yako. Hakika ni huzuni kubwa na inauma sana kumpoteza mpendwa, na hasa pale tunapokumbushwa jinsi maisha yalivyo mafupi na yasiyotabirika.

Maneno yako yametugusa sana na yametufanya tutafakari kwa undani. Ni kweli kabisa, kifo ni ukumbusho mkubwa kwamba hatuna uhakika na kesho, na kwamba kila pumzi tunayovuta ni zawadi. Ujumbe wako wa kuthamini upendo, kusameheana na kuishi kwa amani umefika na ni muhimu sana. Mara nyingi tunasahau thamani ya haya mpaka pale tunapokumbushwa na matukio kama haya.

Tuishi leo kwa upendo, amani na shukrani, tukijua hatujui lini safari yetu itaisha. Mungu akutie nguvu wewe na familia ya rafiki yako katika kipindi hiki kigumu. Rafiki yako apumzike kwa amani.
 
Na utaratibu ambao siupend wa kumpa sifa mtu wakati hayupo huo utaratibu ni mbovu sana na una unafiki ndani yake, mtu aambiwe mazuri yake akiwa hai hiyo itampa thamani ya kuendelea kuishi
Mazuri na thamani ya Mwanadamu vinaonekana akishafariki.
 
😁😁😁 unaogopa kufa au unataka kusema nini tu.Sie wafu,tusisahau kurnjoy hii dunia.
 
Zaburi ya 90
1.wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, Kizazi baada ya kizazi.
2 Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.
3 Wamrudisha mtu mavumbini, usemapo, Rudini, enyi wanadamu.
4 Maana miaka elfu machoni pako Ni kama siku ya jana ikiisha kupita, Na kama kesha la usiku.
5 Wawagharikisha, huwa kama usingizi, Asubuhi huwa kama majani yameayo.
6 Asubuhi yachipuka na kumea, Jioni yakatika na kukauka.
7 Maana tumetoweshwa kwa hasira yako, Na kwa ghadhabu yako tumefadhaishwa.
8 Umeyaweka maovu yetu mbele zako, Siri zetu katika mwanga wa uso wako.
9 Maana siku zetu zote zimepita katika hasira yako, Tumetowesha miaka yetu kama kite.
10 Siku za miaka yetu ni miaka sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Na kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana chapita upesi tukatokomea mara.
11 Ni nani aujuaye uweza wa hasira yako? Na ghadhabu yako kama ipasavyo kicho chako?
12 Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima.
13 Ee Bwana urudi, hata lini? Uwahurumie watumishi wako.
14 Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako, Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote.
15 Utufurahishe kwa kadiri ya siku ulizotutesa, Kama miaka ile tuliyoona mabaya.
16 Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako, Na adhama yako kwa watoto wao.
17 Na uzuri wa Bwana, Mungu wetu, uwe juu yetu, Na kazi ya mikono yetu utufanyie thabiti, Naam, kazi ya mikono yetu uithibitishe.


Tusome 10 na 12
 
Kwenye vitu ambavyo haitakiwi kuviogopa kifo ni kimoja wapo maana ndio kitu cha uhakika hakikwepeki na unakua hujui chochote kama venyewe hujazaliwa tu
 
Back
Top Bottom