Halloo,
Nina rafiki yangu mpenzi jana kanilalamikia kuwa anahisi kuna mtu ana mahusiano ya kimapenzi na mkewe, ila ameshindwa kumkamata kwa sababu saa zote mkewe anafuta message zote kwenye inbox na sent items lakini msg counter inaonyesha kwamba kuna msg nyingi tu zimetumwa.
Naombeni basi kama kuna mtu anajua jinsi au mahali anapoweza kuretrieve hizo message. Simu anayotumia ni ya kichina na line ni ya TIGO.
Please help cause this is serious na jamaa yupo kwenye hali mbaya.
Thanx.
Kwanza mpe pole kwa wasiwasi wake, then mshauri afanye yafuatayo;
1. Asiwe na kifua cha plastic...! Yaani awe jasiri wa kupata ukweli utakaokuwepo...!
2. Ahakikishe kuwa yupo tayari kuyapokea, na anaweza kustahimili maamuzi atakayoyafikia...! Awe na peace of mind...!
3. Ajichunguze yeye mwenyewe, huenda anachangia kuwepo kwa mazingira hayo, then ajirekebishe haraka...!
4. Kisha afanye uchunguzi wa kina, na kwa utaratibu makini, aidha anaweza kufanya haya;
a) Anaweza kukuweka wewe kama PI (private investigator)....!
b) Amwalike huyo mtu nyumbani kwake, then afanye observation...! Things may display automatically...!
c) Kama anamfahamu mkewe vema kisaikolojia, anaweza kumchomekea kama kashtuka, then reactions may indicate the truth...!
d) Ampleke sehemu yenye utulivu, then amrubuni mawazo...! hata kwa kumdanganya kuwa alikuwa na mahusiano na mwanamke fulani, lakini atamwacha, then naye aombe uwazi, huenda ukweli ukapatikana kupitia mdomo wake...!
e) Anaweza pia kumjaribu kumwomba atumie simu yake kwa muda, utayari na uhuru wa mwenzie huenda ikaleta maajabu...!
Vinginevyo, aelewe yafuatayo;
1. Kufumania sio lazima ushuhudie nyoka akiingia shimoni, hata ukimkuta anatoka, ni kufumania pia...!
2. Mwizi wa mbuzi sio lazima umkute zizini, hata akiwa nyumbani kwake, lakini with evidence, ni mwizi...!
3. Ni rahisi kumwamini mbwa aliye zizini na mbuzi, lakini si binadamu...! Hivyo, in this world, "ONLY A FOOL MAY TRUST HIS/HER PARTNER". Bora usishudie...!
4. Normally, but not at all times, feelings comes from some facts, so something might be behind the window...! Awe makini...!