Rafiki yangu anaishi na kaka yake nyumba moja!

Rafiki yangu anaishi na kaka yake nyumba moja!

fadeless

Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
22
Reaction score
1
Habari zenu wadau!

Kuna Dada mmoja nilisoma nae chuoni nikawa nampenda sana,nikamtongoza ila akadai anahitaji muda ili aamue,baada ya muda akaniambia kuwa anahitaji muda zaidi ili amalizie commitment zake huko kwao Shinyanga,kwa madai kuwa anajenga nyumba ya wazazi wake,sasa hivi karibuni December 2010 nilimtembelea nyumbani kwake nikakuta anaishi na kijana mmoja ambaye yeye anadai kuwa ni kaka yake wa damu,alinitambulisha kama rafiki yake wa kiume ila sijawahi(ingawa sijawahi kula tunda),nilipomuuliza kwa nini anaishi nae akasema kuwa siwezi kuelewa sababu ni stori ndefu kidogo ila ndio maana ananiambia kuwa anahitaji muda kurekebisha mambo ya nyumbani kwao,ili tuweze kuwa pamoja,nimejaribu kumshawishi ila inashindikana,sasa siku za karibuni alinipa taarifa ya kuwepo nafasi ya kazi ofisini kwao,niliikataa na nilipokutana nae akanishangaa sana kwa nini nilikataa kazi ile kwa madai kuwa mshahara ni mkubwa sana,alinisalimia kwa mahaba makubwa sana mpaka nikawa naona aibu hasa maeneo yale ya Posta,nikamueleza kuwa bado nasubiri hayo mambo yake yataisha lini akaniambia kuwa nisubiri tu ila nielewe kuwa ananipenda sana na anatamani kuwa na mimi ila majukumu yanambana sana! Naomba ushauri wadau!
 
Changa la macho hilo. Ulipotambulishwa kwa kaka yake alionyesha kufurahi na kukukaribisha?
 
This is Africa bana!...kwanini unaishi kwa speculations?...Unashangaa kuishi na kaka wakati wengine tunaishi na watoto wa shemeji zetu kwa baba wakubwa na wadogo?
 
Jamaa alichukulia poa tu mkuu,akakaa dakika kadhaa kisha akaondoka!
 
kwasisi wazoefu wakula madem wa wa2 apo kiukwel ulipigwa changa la macho,
mi kiukweli nna mchumba wangu kabisaaaa, alafu ninao wengine wawl wa pembeni ambao wao wachumba zao na wanakubali kua nami.. ila wachumba zao wanajua mi ni rafiki yao 2 jinsi walivotambulishwa
 
Anaweza kuwa kaka au mchumba nakushauri ufanye kauchunguzi kidogo kama ni kaka utatambua na kama ni mchumba basi utajua
 
kwasisi wazoefu wakula madem wa wa2 apo kiukwel ulipigwa changa la macho,
mi kiukweli nna mchumba wangu kabisaaaa, alafu ninao wengine wawl wa pembeni ambao wao wachumba zao na wanakubali kua nami.. ila wachumba zao wanajua mi ni rafiki yao 2 jinsi walivotambulishwa

Yaani wewe hili kutuambia huoni hata aibu? Unajua unachokifanya huenda na huyo mchumba wako anakifa , kwa hiyo angalia nini kinaweza tokea katika dunia ya sasa, au unafikiri dawa ya loliondo itabaki kutibu milele?
 
mie hata sijaelewa..............asa weye shida yako ni nini? mara waona aibu?:A S 13:
 
Kila mtu atapewa mwenza wa kufanana nae....... kaka subiri utampata mweza wa kufanana nawe!!!:A S 112:
 
Mkuu kweli hujanielewa,niliona aibu kwa jinsi alivyokuwa ananifanyia movements ambazo zilikuwa zinaletwa muonekano wa kuwa kwamba kwa wakati ule tupo kwenye dimbwi la mapenzi mazito tena mbele ya watu(tulikutana pale Posta pembezoni mwa Postal Bank) hii haileti picha nzuei kwa mtu mwenye heshima zangu!
 
asubiri mwenza wa kufanana nae kwenye lipi embu fafanua sentensi yako


Kila mtu atapewa mwenza wa kufanana nae....... kaka subiri utampata mweza wa kufanana nawe!!!:A S 112:
 
Hujamchunguza vizuri nahisi hauko serious kivile....unapoteza muda....fanya utafiti then amua usuke au unyoe kutokana na findings zako.....!!!
 
Unamsaidia mahitaji yoyote huyu dada? kama unatumia hela kumuonga huyu dada kuna uwezekano mkubwa huyu msela mwingine ni jamaa yake na kashaambiwa wewe ni atm yake, kwahio msela kakubali kutambulishwa kama kaka kwani msaada unaokuja kutoka kwako na yeye unamtoa pia.
 
banaee, kama alikwambia umpe let say mwaka, ukampa.akaomba tena mwingine ukampa na sasa anataka tena mwingine we kua ngamgartu.manak kama yupo siriaz sio wewetu unaemhitaji hata yeye anakuhitaji.hivyo akiona kweli umechoka na umechkua maamuzi magumu atayatoa mhanga hayo anayoayaita majukumu ambayo ndiyo yanyosababisha kukwambia usubiri.
 
Anaweza kuwa kaka au KHAKHA,maana unanikumbusha wakati tuko shule za bweni KHAKHA zetu walivyokuwa wanakuja kutusalimia hahahahahahahhhhhhh:wink2:
 
kudanganya nung'ayembe rahisi kweli, ila kudanganya mwenye akili, vigumu sana...akili za mbayuwayu...changanya na zako.
 
This is Africa bana!...kwanini unaishi kwa speculations?...Unashangaa kuishi na kaka wakati wengine tunaishi na watoto wa shemeji zetu kwa baba wakubwa na wadogo?

mkuu na wengine wanaishi kwa dada zao walioolewa na hakuna noma. Life goes on...
 
kweli love is blind,,,changa la macho hilo....
 
Mi nakushauri ufanye uchunguzi maana chochote chawezatokea. Usikurupuke kama hujui ukweli.
 
Back
Top Bottom