Rafiki yangu kaninunia kisa jina lake limekatwa kwenye kura za maoni

Rafiki yangu kaninunia kisa jina lake limekatwa kwenye kura za maoni

MENEMENE TEKERI NA PERESI

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2022
Posts
5,392
Reaction score
14,646
Salamu sio Sasa labda badae.

Ndugu nasikitika Sana na Sasa nahitaji ushauri maana nipo katika mtanziko wa huzuni na kutia huruma baada ya kunununiwa na rafiki yangu wa hapa kijijini.

Ifahamike kuwa ili wananchi wakuchague kuwa mwenyekiti hasa huku vijijini basi uwe na vihela hela vya hapa na pale ,basi itoshe kuwaeleza kuwa huyu rafiki yangu amekuwa mwenyekiti kwa vipindi au mihula ya miaka ishirini na itoshe kuwaambia kuwa Yuko financially fit ,hivyo jueni nilikuwa na rafiki mwenye vijihela hapa kijijini

Sasa ndugu mwenyekiti mstaafu baada ya habari ya kuchukua fomu katika vyama ili kugombea Tena muhula ujao ,alinitafuta tukakaa sehemu tulivu tukiulizana vipi achukue fomu au aache ni kupitia chama Cha mapinduzi .

Sasa Mimi Kama mtu karibu yake na pia mahauri wake mkuu kwenye Mambo ya siasa na maendeleo yenye tija ,nikatizama watu wanaohitaji kutia nia kupitia chama na pia walivyojiwekea hazina kijijini nikaona rafiki yangu hatoboi .

Nikawaza nikimwambia asichukue fomu hatokubali na tutagombana Sana basi nikaamua Kama mbwa na iwe mbwai nikamweleza kuwa kwasasa umechuja ,chama hakitakupitisha hivyo kulinda heshima yako na yangu hapa kijijini usichukue fomu ,staafu kwa heshima .Alikataa kata kata .

Sasa kwenye kura za maoni basi wanakijiji na wanachama wakambwaga vibaya hovyo rafiki yangu.

Jioni baada ya kumwagwa nikajipa muda walau nikampe pole rafiki yangu na hapo nimjaze kichwa aanze kufanya utaratibu wa kupata kiti Cha udiwani ,nikamkuta nyumbani kwake na mkewe ila Yuko na hasira ,salamu na stori ambazo hazihusiani nisije kumtibua na mwisho nikaaga nikaondoka zangu.

Sasa Leo nikiwa klabuni ndiyo taarifa zikatibolewa na mwanakijiji mbeya kuliko wote kuwa mwenyekiti mstaafu amesema hanipendi na anajua fika Mimi ndiye niliyemuhujumu ,ukiangalia Sina uhusika wowote katika kumpitisha mtu kichama ,Basi roho ikawa imeniwaka Moto, kiguu na njia mpaka kwa rafiki yangu nikajue yasemwayo Yana ukweli au ni mbilinge za waja kuvunja urafiki wetu.

Doh chair si kanitimua kwake ati hanipendi na Wala hatamani kuniona Mimi ni mnafiki kwakuwa nilipanga njama za yeye kubwaga chini ,amebwatuka Mambo mengi mbele ya wake zake mpaka habari za kwenda kununua tudada mjini eti Mimi ndiye uwa namshawishi na pia sio rafiki mwema.

Ndugu zangu wanajamiiforums ,kiukweli huyu ni rafiki tuliyeshibana Sana hapa kijijini na naweza kusema ni mtu namkubali ila kuanza kusema Siri zetu mbele ya wake zake kiasi Cha kuonekana Mimi ndiye namshawishi ujinga kimeniuma Sana ,nikajaribu kumpigia simu walau tuzungumze ili hata Kama ukaribu haupo ila aache lawama na kusema yaliyopita na simu anakata.

Itoshe kusema nimekasirika sana na pia nimeumia Sana ila zaidi kunishitumu Mambo ya tudada mbele ya wakeze na vile walivyokuwa wananiheshimu basi nimejihisi vibaya mno.

Sasa naomba ushauri nifanyeje kumaliza huu utata kwa amani hata urafiki ukifa sawa ila sio habari za kutangaza Siri zangu.

Karibu
 
H
Kwani wewe ndio mkataji?
Hapana Mimi ni rafiki yake mkuu na mshauri wake mkuu wa masuala ya kisiasa na maendeleo yenye tija hapa kijijini ,kosa ni kuwa niliona kabla kuwa rafiki hatoboi Sasa hakupenda Mimi kumwambia ukweli
 
Kuna mmoja hapa kaukosa ujumbe basi kila mtu anamuona mbaya,
Na sasa ameanza kunywa vijuis vile vya glass
 
Back
Top Bottom