GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
GENTAMYCINE (Shabiki Tukuka wa Simba SC) nilishawahi kuandika Mada (Thread) hapa hapa JamiiForums ya Kuwaonya akina Inonga na Sakho juu ya Uchezaji Wao wa anao anao mwingi na kutafuta Sifa kwa Majukwaa huku Nikionya kuwa ipo Siku yatawakuta makubwa.
Sikueleweka na baadhi ila nina baada ya Tukio la leo sasa nitaeleweka vyema na ikibidi hata kupigiwa Salute kwa kuwa Critical Observer na Mwana Maono niliyebarikiwa na Mwenyezi Mungu.
Rafu ya Kwanza
Kulikuwa na haja gani ya Inonga Kukokota Mpira kiasi kile wakati akina Kapombe, Sakho na Saido walikuwa mbele yake na angewapa tu Pasi ili abaki salama?
Rafu ya Pili
Vitu vingine ni Football Intelligence tu. Hivi umeshajua tayari kutokana na Rafu ya Kwanza kuwa Mshambuliaji fulani amekudhamiria Kukuumiza kulikuwa na haja gani unaona unaenda nae katika One to One tena ya Sliding na Wewe unajiingiza mazima mazima kwa kuzama nae Uvunguni?
Na hapa wana Simba SC Wenzangu mliopo JamiiForums mtanisamehe GENTAMYCINE ila pamoja na kwamba Kibinadamu (Emotionally) nimeumia kwa Kuumia Kwake ila upande mwingine Nimefurahi kuwa acha aumizwe vile ili Kumsaidie Kumsthtua na hata Kumrekebisha pia ili akipona na Kurejea tena Uwanjani awe na Adabu na apunguze Sifa, Ushamba na Utoto wake ambao Binafsi huwa Unaniboa sana tu.
Mbona Beki wa Yanga SC na MVP wa Ligi Kuu iliyomalizika Yannick Bangala ni Mchezaji mzuri, mahiri na wa Kutegemewa kabisa ila hana Upuuzi huu alionao huyu Mkongomani Mwenzake Henock Inonga Baka?
Kwanini Inonga hataki au hawezi Kujifunza kutoka kwa Clatous Chama ambaye ana Football Intelligence ya hali ya Juu na inayomsaidia asichezewe Rafu au asijihatarishie Kuchezewa Rafu Mbaya?
Chama huwa anapiga Chenga au anafanya Mbwembwe zake pale tu inapobidi ila akiona anaocheza nao ni Wahuni na Wakorofi mara nyingi huwa anagusa tu na kuachia mara moja na kujikuta anamaliza Mechi salama na amekuwa akifanya hivyo sana tu.
Mwisho GENTAMYCINE namalizia kama Inonga au Wana Simba SC mliopo hapa JamiiForums mtachukia kwa Kilichotokea/Kilichomtokea leo Beki Inonga na Kulaumu hebu tukiacha Unafiki na tukimuogopa Mwenyezi Mungu hivi kwa mfano ile Rafu Mbaya ya Inonga aliyomchezea Kiungo wa Yanga SC Salum Aboubakary 'Sure Boy' ingempata vilivyo leo hii angekuwa anacheza Mpira?
Mwmbieni Inonga Muosha nae Huoshwa hivyo awe Mpole kabisa, auguze Jeraha lake na asiinue Mdomo wake Kulaumu kwani kama Yeye leo alivyohatarishiwa Career yake basi nae pia angehatarisha vile vile na Career ya Mwenzake 'Sure Boy' wa Yanga SC hivyo atulie tu.
Nililolitegemea leo limemtokea live!!!