Rage atapeli Ze Comedy-Tabora!

Zyansiku

Member
Joined
Jul 27, 2009
Posts
49
Reaction score
10
Aliyewahi kuwa katibu mkuu wa TFF(FAT wakati huo) Alhaj Ismail Aden Rage ametapeli kiasi kikubwa cha fedha katika onyesho maalumu la kikundi cha wachekeshaji Ze comed. Bwana rage ambaye pia ni M/kiti wa jumuiya ya CCM ya wazazi mkoani Tabora alitapeli kiasi hicho cha fedha kwa kuingia mitini na kutokomea baada ya show hiyo katika ukumbi wa VOT Club (Rufita club) awali ilidaiwa kuwa bwana rage aliingia mkataba na Bwana yusuf Kitumbo ambaye ndiye aliye wadhamini Ze Comed na kuwalipa kiasi chao cha fedha, bwana Rage ambaye mawasiliano yake na Benki siku hizi si mazuri naye akamuomba bwana kitumbo ili aongee na Ze comed ili baada ya show ya mchana ze comed watumbuize kwenye club ya VOT , bwana rage hakuwa na kiasi cha fedha kama advance kwa ze comed hivyo kulazimika kuahidi kuwa mara baada ya show atalipa kiasi hicho cha fedha kwa bwana kitumbo ambaye ndiye mdhamini mkuu wa ze comed kwa Tabora tatizo lilikuja pale bwana Rage alipokusanya fedha na kuingia mitini! masweali ya kujiuliza kwa watu wa mji wa Tabora bwana Rage kwa madhaifu hayo ataweza kuwa Mbunge wa Jimbo la Tabora?
 
hii imekaa kimipasho sana ...mamabo ya kuwa rage hana mahusiano mazuri na benki yanatoka wapi..typical ze utamu thing...
 
hii imekaa kimipasho sana ...mamabo ya kuwa rage hana mahusiano mazuri na benki yanatoka wapi..typical ze utamu thing...

Ina muonekano wa kuharibiana kisiasa zaidi ni kama chuki flani vile.
 
Mkuu Mvina tuko ukurasa mmoja.Unajua sometimes mi naona mpaka hii forum inapoteza maana.hatuwezi kukaa tunajadili mambo substantial na ya msingi kama ilivyokuwa zamani.yaani ni majungu tupu mara rage katapelo ze comedi,mara mh.mdee ni lesbian mara sijui nini.yaani nahisi kutapika
 
hawa ni wapinzani wa kisiasa wa rage kwa hiyo wanajaribu kupenyeza ujinga wao hapa JF. Uzuri wa JF members ni critical na hatukawizi kuwapa vidonge wote waleta majungu na fitna za ki-RA.

Mkuu Zyansiku, tafadhali fanya utafiti wa habari yako kabla hujaitundika hapa JF vinginevyo na wewe utakuwa sawa na mtu mmoja najiita engineer humu JF.
 

Kigogo nimekuelewa hii mada kweli imekaa kishigongo sana kutakuwa na mkono wa wapinzani wake kisiasa kwanini mtoa maada mwisho anamaliza kwa kuhusisha hili na politics!
This is kind of political waterloo.
 

SASA ALIYETAPELIWA ni ZE COMEDY AU YUSUPH KITUMBO?
 
kumbe mpo wengi wambea wambea, hizi habari si mahali pake
 
huku ni kumdhalilisha mtu, age hawezi akakimbi tabora kwa deni la ze komedi, mimi ninachojua gharama za kupata ubunge ni zaidi ya m50, sasa mtu kama anafikia kutaka kugomea it means anazo pesa za campain
 
Peleka gazeti la sani

huku ""hatudanganyiki" kirahisi
 
Hii habari iwe kimipasho au vyovyote mtu aonavyo, RAGE NI MCHAFU KIMAADILI NA HAPASWI KUCHAGULIWA KUWA MBUNGE WA JIMBO LOLOTE NCHI HII (KAMA KWELI ANA NIA HIYO).
 
This kind of habari zinaidhalilisha forum yetu. Moderator please do something, tuwe critical in discussing only developmental issues and not people!!!!!

Utakosa wachangiaji tukikosa kulitazama hili kwa jicho stahili!!!
 
huku ni kumdhalilisha mtu, age hawezi akakimbi tabora kwa deni la ze komedi, mimi ninachojua gharama za kupata ubunge ni zaidi ya m50, sasa mtu kama anafikia kutaka kugomea it means anazo pesa za campain

JF ni mahali pa heshima sio mahali pa kupenyeza kampeni uchwara za ubunge wa chama cha mafisadi! Maadam mmeanza kumuandika Rage nyie wanyamwezi sasa hivi wengine wataleta ya Kaboyonga. Kaeni na siasa zenu za kifisadi huko huko unyanyembe.
 
Please Magazeti ya Udaku hatuyataki humu, We need fact issues.
 
kwani onyesho moja la ze comed ni kiasi gani? kama sio kudhalilishana,mwacheni Rage aendelelee na kampeni zake za ubunge wa Tabora mjini-msimchafue.
Habari hii si kweli -atudanganyiki na udaku huu.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…