Aliyewahi kuwa katibu mkuu wa TFF(FAT wakati huo) Alhaj Ismail Aden Rage ametapeli kiasi kikubwa cha fedha katika onyesho maalumu la kikundi cha wachekeshaji Ze comed. Bwana rage ambaye pia ni M/kiti wa jumuiya ya CCM ya wazazi mkoani Tabora alitapeli kiasi hicho cha fedha kwa kuingia mitini na kutokomea baada ya show hiyo katika ukumbi wa VOT Club (Rufita club) awali ilidaiwa kuwa bwana rage aliingia mkataba na Bwana yusuf Kitumbo ambaye ndiye aliye wadhamini Ze Comed na kuwalipa kiasi chao cha fedha, bwana Rage ambaye mawasiliano yake na Benki siku hizi si mazuri naye akamuomba bwana kitumbo ili aongee na Ze comed ili baada ya show ya mchana ze comed watumbuize kwenye club ya VOT , bwana rage hakuwa na kiasi cha fedha kama advance kwa ze comed hivyo kulazimika kuahidi kuwa mara baada ya show atalipa kiasi hicho cha fedha kwa bwana kitumbo ambaye ndiye mdhamini mkuu wa ze comed kwa Tabora tatizo lilikuja pale bwana Rage alipokusanya fedha na kuingia mitini! masweali ya kujiuliza kwa watu wa mji wa Tabora bwana Rage kwa madhaifu hayo ataweza kuwa Mbunge wa Jimbo la Tabora?