Msidanganyike waungwana kuwa na nyumba ndogo ni upuuzi na mzigo tu, katika ulimwengu wa sasa sidhani kama kuwa na multiple relationships ni deal, sana sana unaandaa mazingira ya kuja kuitesa familia yako tu baadae, kwanini uwe na nyumba ndogo wakati ulishakula kiapo cha uaminifu kwa mkeo, kama ni hizo stress kwani hakuna njia nyingine ya kuzishusha zaidi ya kwenda kenye nyumba ndogo?..Nionavyo mimi kuwa na nyumba ndogo ndiyo kuzidi kujikaribishia maradhi zaidi kwani most of the time utakuwa kwa mkeo sasa huu muda ambao hauko na nyumba ndogo yako unajua yeye anafanya nini huko pembeni?..hili ni dogo, kubwa zaidi ni kuwa utakapokuwa ma watoto wa nje huoni kama utawatesa hawa watoto bure, mimi huwa naamini kuwa mapenzi kati ya watoto huwa ni makubwa zaidi kama watoto ni wa tumbo moja kuliko kuwa wa mama tofauti, sasa huoni kama utawapa shida tu watoto wako...
Mtu asiseme kuwa eti ooh kwani ni lazima nizae na huto nyumba ndogo, asikudanganye mtu ndugu yangu utategeshewa wewe utagonga, mimba itatunga na mtoto utamlea bila kupenda..,kuna wanawake wapo kiuchumi zaidi wewe asikwambie mtu.