Raha ya safari za usiku 12Hrs Dar - Shinyanga

Raha ya safari za usiku 12Hrs Dar - Shinyanga

Interesting
Vipi hao jamaa mlio ongozana nao, ulipata mrejesho wowote nini kiliwasibu?
Ndio nilipata mrejesho kwenye izo gari mbili zilizonitangulia kulikua na mwamba anamzigo mrefu uwa anafata ng'ombe kwenye minada anapakia kwenye roli analeta Dar,sasa naona jamaa kumbe walikua wakimfatilia bila yeye kujua.

Jamaa waliotekwa wanahadithia waliposimamisha gari waliwashusha chini wakawalaza wakawasachi lakini yule mwenye hela walisimama nae pembeni wakiwa wameshamnyang'anya begi simu na kilakitu.
Walimchapa risasi ya mguu moja,wakachapa risasi tatu gari ya mbele zilifika kwenye boneti na shoo ya mbele ili dereva asimame.
Jamaa wanahadithia laghfidh ya watekaji sio ya kitanzania ina asili ya uko nchi za jirani,Congo,Burundi au Rwanda.
Jamaa wanahadithia askari waliokua upande wa kutokea Ushirombo waliwai kufika mapema baada tu ya kupata taarifa lakini jamaa walikua washaingia vichakani huko.
 
2009 nilikoswa koswa kutekwa pori la Runzewe usiku kwa ubishi tu,askari uwa wanaweka beria kuzuia gari zisipite usiku kuna majambazi wanatekaji kwenye ilo pori.
Wabishi tulikua jumla gari tatu tukapeana moyo tutasindikizana tukatoa posho,askari wakatutahadharisha kabisa kuna hatari huko usiku sio salama lakini atukusikia.
Safari ikaanza wenzangu wawili wakakamua mafuta mimi na pajero ya urithi nikawa naenda mwendo wa kunyata.

Katikati ya pori kuna konakona umo,kumaliza kona flani hivi nikapiga taa full nikaona watu barabarani na zile gari mbili zimesimama moja ikiwa pembezoni mwa barabara.kumbe tayari wenzangu wamekutana na magogo barabarani,nikasimama kwa mbaali sasa ili nisome kuna nini!!
Majambazi wakajua gari nililosimamisha ni askari wakaanza kurusha risasi huku wakijihami.
Nikaingia porini kidogo nikachekecha gari nikageuza kurudi bila madhara ya risasi kunipata mimi na gari.
Wakati huo kuna dada nimempa lifti siti ya nyuma akanikaba shingoni kwa uwoga tu.

Tangia siku hiyo nikashika adabu kutembea usiku.
Bhana w October tu hapa tumepita Runzewe sa tank hivi tuko ndan ya Gari MTU mbili tu, Ushirombo wadau walisema tulale pale sie tukakomaa tu ila hofu m yake sio ya kitoto
 
Saa 9 kasoro usiku..pale panahitaji umakini tu hasa kwa sababu ukiwa unashuka panakuwa kimyaa sana kona nyingi kali na mteremko wa kutisha..nilitembea 80 tu pale
Ila kuna watu mnatembeza gar aisee..yaan 80 kushuka kilima kama hiko unasema ni speed ya kawaida?tena usiku.....plus unasema ulikua unakamua 100-120..mim siwez endesha gar speed hzi aisee..napenda sana uzinz na kula bata bado
 
Bhana w October tu hapa tumepita Runzewe sa tank hivi tuko ndan ya Gari MTU mbili tu, Ushirombo wadau walisema tulale pale sie tukakomaa tu ila hofu m yake sio ya kitoto
Tushapita ushirimbo usiku kuna mahali tukaona gari imapaki pembeni, kwenye gari kila mtu akawa kimya kwa hofu.
Nilikuja kupata amani baada ya kufika Kahama.
 
Wasalimie Ngokolo,Mwasele,Ushirika, Ndala,Upongoji,Ndembezi,Old Shy,na miss sana pande za Shy Town [emoji122][emoji122]
Nimetoka shy juzi..wako poa sana mvua inavyesha ingawa imechelewa..wanakusalimu pia usiache kwenda xmas.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ila kuna watu mnatembeza gar aisee..yaan 80 kushuka kilima kama hiko unasema ni speed ya kawaida?tena usiku.....plus unasema ulikua unakamua 100-120..mim siwez endesha gar speed hzi aisee..napenda sana uzinz na kula bata bado
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] kawaida mkuu
 
Nina experience mbaya na safari za usiku, 2016 tulitekwa na wale wa kuweka magogo barabarani kati kati ya Same na Mwanga.
Safari ilikua Arusha to Dar, tulitoka Arusha sa 6 kasoro usiku, waliharibu sana gari kwa kuvunja vioo ila tunashukuru hawakutudhuru hata zaidi ya kutuchukulia vitu vyetu.

Ilinichukua muda kidogo kupona ile hofu ya lile tukio na nimekua muoga hadi leo wa kusafiri usiku.

Hahaa nakumbuka baada ya lile tukio hata sherehe za usiku nikastop kuhudhuria almost a year maana likiingia giza kama sijarud home hofu inatanda😅
Nipe kazi ya bodyguard basi hofu itaisha.
 
Wese la laki2 wakati ungepanda bus ungetumia less than 60K
Bus haitembei usiku kama anavyotaka yeye, kifupi ukiwa na gari binafsi ina raha yake uko flexible na unafuata ratiba zako utakavyo. Pili ukiwa na familia bus ni gharama zaidi kulinganisha na private.

Mfn. Unatoka Dar unaenda Shinyanga mko watu Ludewa gharama za kula, kulala, na nauli ni kubwa kulinganisha na kusafiri na private.
 
Ila kuna watu mnatembeza gar aisee..yaan 80 kushuka kilima kama hiko unasema ni speed ya kawaida?tena usiku.....plus unasema ulikua unakamua 100-120..mim siwez endesha gar speed hzi aisee..napenda sana uzinz na kula bata bado
Hahaha njia ukiijua ndiyo inakuwa poa sana halafu mbona hiyo speed ni ndogo sana
 
Back
Top Bottom