Rahma Kisuo: Mkiongeza Kodi kwenye 'Betting' tutaua ajira

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mbunge wa Viti Maalum, Rahma Riyadh Kisuo, ameonya kuwa ongezeko la kodi kwenye sekta ya michezo ya kubahatisha linaweza kuathiri shughuli za biashara na kusababisha kupotea kwa maelfu ya ajira nchini.

Akichangia mjadala wa Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2025 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027, Kisuo amesema Serikali inapaswa kuangalia kwa makini athari za ongezeko hilo kabla ya kulitekeleza.

Amesema iwapo kodi ya asilimia tano itaongezwa, ni vyema ikaelekezwa kwanza kwenye michezo ya kubahatisha inayofanyika mtandaoni kuliko kwa waendeshaji wa vituo vya michezo ya kubahatisha (retail-based betting).

“Mimi nashauri ongezeko la kodi la asilimia tano lianze moja kwa moja kwenye internet betting kwanza. Likipelekwa kwenye retail-based casinos tunakwenda kuua kabisa operesheni za biashara hizo,” amesema.

Kisuo amesema sekta hiyo kwa sasa inatoa ajira zipatazo 2,000 za moja kwa moja na zaidi ya ajira 4,000 zisizo za moja kwa moja, hivyo ongezeko la kodi linaweza kuathiri uwezo wa waendeshaji kuendelea na shughuli zao.

“Tunapokwenda kuongeza kodi tunakwenda kuua operesheni, na tunapoua operesheni tunakwenda kuua ajira zaidi ya elfu nne,” amesema.

Soma pia Serikali kuweka Tozo ya 5% kwenye 'Betting' kuanzia Julai 2026, kuzuia Uraibu wa Vijana

asiongeze ??? halafu RAIS wa MAWE atapata wapi pesa za kupiga!
 
Back
Top Bottom