RAI: Wasanii Tuzo wajifunze kuwaheshimu wapinzani

RAI: Wasanii Tuzo wajifunze kuwaheshimu wapinzani

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
20,834
Reaction score
26,217
Hafla ya utoaji wa Tuzo za Muziki za Tanzania (KTMA) 2015 iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi usiku iliwavutia wengi.

Mamia walihudhuria tukio hilo na mamilioni wakashuhudia yanayojiri ukumbini kupitia matangazo ya moja kwa moja ya televisheni yaliyorushwa na vituo viwili kikiwamo cha ITV.

Lilikuwa tukio kubwa. Mandhari ya ukumbi ilipendeza. Mfululizo wa burudani zilizotolewa jukwaani na wasanii pamoja na watangazaji wazoefu waliokuwa wakisherehesha, uliwafanya wengi wachangamke muda wote.

Burudani iliyotolewa na wasanii Christian Bella, Vanessa Mdee, Weusi na wengine, iliufanya usingizi ukose nafasi kwa walio wengi, ambao walifuatilia kuanzia mwanzo hadi usiku wa manane wakati washindi wa kila kipengele walipojulikana.

Wasanii waliofanya vizuri zaidi kwa kutwaa tuzo nyingi ni pamoja na Ali Kiba aliyeibukakinara kwa kuchomoza katika vipengele sita, akifuatiwa na Vanessa Mdee, Mzee Yusuf na Diamond Platinumz (3).

NIPASHE tunawapongeza washindi wote wa mwaka huu wa tuzo hizo.

Tunaamini kwamba jitihada zao katika kuandaa nyimbo zenye ujumbe unaogusa jamii, kuwa na mapigo ya kuvutia, kuzingatia maadili na pia kuandaliwa video zenye ubora wa hali ya juu ni miongoni mwa sababu nyingi za wao kuwa vinara. Hongera kwa wote.

Hongera pia kwa wale waliofika katika hatua ya mwisho ya mchujo na kukubali kushindwa, wakiamini kwamba hawapaswikukata tamaa bali kujipanga upya ili wafanye vizuri zaidi mwakani.

Pongezi nyingi pia ziwaendee waandaaji. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mchakato wa shughuli yenyewe huambatana na uwekezaji mkubwa wa rasilimali, muda na fedha.

Ni jukumu kubwa linalohitaji kuwa na dhamira ya dhati ya kuendeleza muziki.Hata hivyo, wahenga husema penye zuri hapakosi kasoro.

Licha ya kuwapo kwa mambo mengi mazuri katika siku ya utoaji tuzo, bado kulikuwa na baadhi ya mambo yaliyowakera wengi.

Na kubwa kuliko yote ni pamoja na kitendo cha kutokuwapo ukumbini kwa baadhi ya wanamuziki wateule wa kuwania tuzo na maneno ya shombo yaliyotolewa na baadhi ya washindi.

Wateule kutokuwapo kwenye eneo la tukio kulionekana kuwakwaza wengi, hasa pale majina yao yalipotajwa kuwa ni washindi, wakakosekana na kutuma watu wengine kupanda jukwaani kwa niaba yao.

Wanamuziki wenye mtazamo wa mbali huwa hawakosekani kwenye hafla kama yajuzi.

Ushiriki wao huongezeka maradufu pale wanapojua kuwa nao ni miongoni mwa wale wanaowania tuzo hizo.

Jambo lililoshangaza na kukera zaidi ni pale baadhi ya washindi walipotoa majigambo na vijembe dhidi ya waliowashinda.

Sisi tunaamini kwamba kitendo hiki hakikustahili kwani ni kutowatendea haki waandaaji na mashabiki waliowapigia kura.

Mathalan, viongozi wa makundi ya Jahazi Moderm Taarab na Mashauzi Classic, Mzee Yusuph na Isha Mashauzi, walishambuliana kwa vijembe na majigambo ambayo tunaona hayakupaswakuonyeshwa katika tukio muhimu kama la juzi.

Mbaya zaidi, Mzee Yusuph alifikia hatua ya kuwabeza waimbaji wote wa taarab nchini akieleza kuwa wapinzani ambao kidogo wanaonekana nyuma yake ni Isha Mashauzi na Thabit Abdul, lakini 'wengine watasubiri sana kwa sababu Jahazi iko juu na itaendelea kuwa juu.

'NIPASHE tunatambua uhasama uliopo baini ya makundi ya muziki wa taarab nchini, lakini tunazidi kusisitiza kwamba katika tukio kama la juzi waimbaji hao hawakupaswa kutupia vijembe na kutoa majigambo ambayo si tu yaliwashusha hadhi wao wenyewe, bali yalitoa taswira mbaya kwa tasnia ya muziki wa Tanzania na tuzo hizo kwa ujumla.

Ni wanamuziki wa kundi hili ndiyo tusiowaunga mkono na kuwataka wabadilike kwani tuzo za aina hii zinapaswa kuenziwa na wao wenyewe na si kuzigeuza sehemu ya mipasho isiyokuwa na tija.

Linapofika suala la tuzo, wasanii na wadau wengine wa tasnia ya burudani hawana budi kuwaheshimu wapinzani wao kwani bila wapinzani, hakuna ushindani.Klabu ya Barcelona ya Uhispania ni mfano mzuri kwa hili.

Wachezaji na maofisa wa klabu hiyo wamefunzwa kuheshimu wapinzani wao.

Hata wakishinda magoli mengi, bado wataonyesha ishara ya kuwaheshimu wapinzani wao.

Shime, wanamuziki wetu waamke. Wajifunze kuheshimu wapinzani wao kwa manufaa yao na fani yao.

CHANZO: NIPASHE
 
Yaani kama mzee Yusuph alinikera sana!kulikuwa na haja gani ya yeye kuropoka kiasi kile?eti tuzo imeenda mahala pake,yaani anajiamini kupita maelezo
 
Jamani hata mbele iko hivyo,Bet kwa sana tu huo upuuzi upo. Nadhani ndio tabia/ hulka yetu ngozi nyeusi. Mwisho wa siku,ujumbe ni ule ule usichukie ila hamasika ufanye mazuri zaidi.
 
Yule wa FM Academia ndiyo pekee alisema vzr kuwa Twangapepeta ni bendi nzuri,Mashujaa ni bendi nzuri,Mapacha ni bendi nzuri lakini wao wamekuwa na bahati ya kushinda.
 
Back
Top Bottom