Rai ya Mzee Aboud Jumbe kwenye Kitabu Chake Tuishi Bila Kubaguana

Bukanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2010
Posts
2,857
Reaction score
1,938
Ukiachilia mbali kitabu chake cha THE PARTNERSHIP, Mzee Aboud Jumbe Mwinyi, aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu Wa Kwanza wa Rais wa Tanzania kabla ya kushinikizwa kujiuzulu na chama mwaka 1984 kutokana na msimamo wake wa serikali tatu, ameandika pia kitabu kingine kinachoitwa TUISHI BILA KUBAGUANA.

Kwenye kitabu hicho kilichochapishwa mwaka 2003 Mzee Jumbe anaeleza mengi kuhusu kuvuliwa kwake nyazifa za uongozi kwenye chama na serikali. Fuatana nami nikupe machache;

KIKAONI DODOMA

"…Siku tatu za kwanza za mkutano, Jumanne hadi Alhamis, ni wajumbe wachache tu, wote wakiwa kutoka Tanzania visiwani, ndio waliosimama mmoja baada ya mmoja kulalamika na kushambulia kule walikokuita 'kupenda kwangu na kunyima madaraka, kutosikiliza shauri wala maoni, kujifanyia nitakavyo, kutoipenda CCM na Azimio la Arusha na madai mengine kama hayo'…" ( uk 15)

KUJIUZULU

"….Siku ya Jumamosi, baada ya kumuachia Ramadhani Haji (aliyekuwa Waziri Kiongozi) kutoa maelezo yake, ndipo mimi nilipochambua tuhuma zilizotolewa. Nilipomaliza nikashauri niruhusiwe kuacha shughuli zote za chama na serikali"

BAADA YA KIKAO

"….Nilipowasili nilikofikia, si muda walifika Mabwana Kawawa na Sokoine wakifuatiwa muda mfupi na Mwalimu Nyerere. Niliambiwa kwa vile niliacha madaraka kwa mdomo hakuna ushahidi, bora kufanya uthibitisho kwa maandishi.
Kwa kutotaka 'kuchafua hali ya hewa' niliandika kuacha madaraka ya Makamu Mwenyekiti wa chama na Makamu wa wa Rais wa Muungano, nikampa aliyekuwa mpiga taipu wangu achape. Mwalimu aliponiuliza kuhusu Zanzibar nilimwahidi kufanya hivyo nikifika Zanzibar"

HAIFAI KWENDA ZANZIBAR!

"...Hapo ndipo aliponiambia ingekuwa bora kwa 'sasa' kutokwenda Pemba (Nilikotaka kumpeleka kwao mke wangu niliyekuwa nimefuatana naye ) wala kwenda Unguja na kwa hiyo niandike na kuacha kwangu shughuli za Zanzibar. Kwa kuona wazi wasiwasi uliojidhihirisha, nilikubali yote."

ULINZI MKALI

"...Tulipofika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam na kukuta ulinzi mkali wa Jeshi na Polisi, wakiwepo mkuu wa jeshi na mkuu wa jeshi la polisi, nilishindwa kabisa kuelewa sababu na maana ya yote hayo yalikuwa ni ya nini au kwa nini? Mpaka leo hakuna aliyenielimisha na bado niko ujingani" (uk 17)

SIMU IMEKATWA!

"....Nilipwerewa nilipofika nyumbani Mjimwema na kutaka kupiga simu Unguja. Niliona, kabla ya kutangazwa yaliyotokea, niwatulize wake zangu na wanangu Unguja angalau wajue tu nilikuwa salama Mjimwema. Niligundua simu hazifanyi kazi! Hapo nilimshukuru Mwenyezi Mungu nikamwachia yeye na kukaa kusubiri maajabu mengine huku nikiwaza 'Tunakwenda wapi'?"

SERIKALI TATU

"....Mfumo wa serikali tatu ndio umekuwa msimamo wangu na ndio mtizamo wangu uliopingwa vikali na chama..."

MAHUBIRI YA KUUVUNJA MUUNGANO!

"....Wenye kuhubiri kuuvunja muungano, watambue kuwa hawawezi kufanya hivyo kienyeji… Huu ni muungano wa Watanzania, si wa chama hiki au kile. Wote wenye umri wa miaka ishirini na tisa na chini ya hapo ambao naamini ndio wengi, hawajawahi kuwa chochote isipokuwa Watanzania.
Kabla ya kuwanyang’anya au kuwafutia utanzania wao, wana haki ya kushirikishwa kuamua nasaba yao. Hii inamaana itapaswa kufanyika kura ya maoni ili Watanzania wenyewe ndio waamue kuvunja au kubadili mfumo wa Muungano.
Kisheria na kwa mujibu wa katiba, si jambo dogo au jepesi kuvunja Muungano, kama inavyoonekana baadhi ya viongozi kudhani. Lazima Watanzania kuangalia, kutafakari kwa makini na kujuana kwa yakini tunatoka wapi, kwa nini tuliungana, tumefika wapi na sasa tunataka au hatutaki nini, au tunataka kwenda wapi."

RAI YAKE

"....Katika zoezi hili (kuhusu Muungano), wanasiasa na Watanzania kwa ujumla wanapaswa wawe wakweli, wenye busara na zaidi kuliko yote ni uaminifu. Miaka 100 ijayo hapatakuwa, sio tu katika hili bali kote duniani, hata mmoja miongoni mwa walio duniani leo na hata akiwepo hatakuwa na lake. Bali, vizazi vyetu vitakuwepo. Mazao ya mbegu tunazoatika au kupanda leo itabidi kuvunwa na vizazi vyetu kesho"

Kwa uchambuzi/simulizi kuhusu vitabu na waandishi endelea kutembelea ukurasa wetu wa "Kitabu Nilichosoma" ili upate kujifunza zaidi.
..........
**Post hii iliandikwa yapata miaka miwili Iliyopita. Mungu amlaze pema Mzee Jumbe.
Ndugu Ado Shaibu
Simu: 0653619906
Baruapepe: adoado75@hotmail.com
14.08.2016
 
"….Siku ya Jumamosi, baada ya kumuachia Ramadhani Haji (aliyekuwa Waziri Kiongozi) kutoa maelezo yake, ndipo mimi nilipochambua tuhuma zilizotolewa. Nilipomaliza nikashauri niruhusiwe kuacha shughuli zote za chama na serikali"
Wale ambao siku zote wamekuwa wakidai kuwa alilazimishwa na Mwalimu Nyerere kujiuzulu nyandhifa zake waje hapa watuambie kwamba maneno haya Mzee Jumbe alilazimishwa na nani kuyaandika kwenye kitabu chake?
 
Inaonekana nafasi ya Raisi wa Zanzibar alilazimishwa kujiuzuru kabla hata hajaenda zanzibar
 

Naona wewe ni mtafiti mzuri. Unaweza pia kufuatilia na kuandika historia nzuri ya viongozi wa nchi wengi tu. Unaweza kuchunguza maisha ya Mh Rashid Mfalme Kawawa na mahusiano na mke wake Marehemu Sofia Kawawa, kama hivi unaendelea na Mwl n.k, Hawa walikuwa wajamaa wazuri.
 
Wale ambao siku zote wamekuwa wakidai kuwa alilazimishwa na Mwalimu Nyerere kujiuzulu nyandhifa zake waje hapa watuambie kwamba maneno haya Mzee Jumbe alilazimishwa na nani kuyaandika kwenye kitabu chake?
Soma maelezo chini ya sub headings:

BAADA YA KIKAO

HAIFAI KWENDA ZANZIBAR
 
Mkuu soma mstar kwa mstar Acha kukimbia comment
Nimesoma na nimeelewa. Ilikuwa ni wakati wakubadilishana madaraka katika njia ambayo ilikuwa haijawahi kutokea Zanzibar. Kwa bahati nilipata fursa ya kujua kilichotokea kwenye kikao alichojiuzulu Jumbe!
 
Wale ambao siku zote wamekuwa wakidai kuwa alilazimishwa na Mwalimu Nyerere kujiuzulu nyandhifa zake waje hapa watuambie kwamba maneno haya Mzee Jumbe alilazimishwa na nani kuyaandika kwenye kitabu chake?
Mkuu, sio miimi wale wewe unaye jua ukweli kuhusu hayo mambo, ukweli wanujua wenyewe na MUNGU, ila la muhimu zaid kama uliwafanyia watu mabaya na yakuchukiza nibra uwekaribu na Mungu mapema kabla mda haujaisha.​
 
Natafuta kitabu chake cha " The Partnership: miaka 30 ya Dhoruba " kwa anayejua vinapopatikana wakuu...

Shukran.
 
Nimesoma na nimeelewa. Ilikuwa ni wakati wakubadilishana madaraka katika njia ambayo ilikuwa haijawahi kutokea Zanzibar. Kwa bahati nilipata fursa ya kujua kilichotokea kwenye kikao alichojiuzulu Jumbe!
Kama ulibahatika kujua kilichotokea ni vyema ukatujuza ili kuongeza ufahamu mzuri wa Maisha ya Aboud Jumbe
 
KWEZISHO Nitakuwekea hotuba ya Mwalimu ndiyo utajua alichokisema Seif Sharrif Hamad kama kilikuwa ni cha kweli au uongo.
 
Je suala la Jumbe linafanana na la Nchimbi?
 
Je suala la Jumbe linafanana na la Nchimbi?

Halifanani bali ni KISASI
Wenzetu wako wazi kuhusu nchi yao kuwa na mamlaka kamili, ccm imekaza fuzu na kuna mwanya kwenye katiba.

Sasa wanaitumia effectively kutunyoosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…