mcheza ngoma
New Member
- Sep 2, 2021
- 3
- 1
Uchumi na Biashara
Serikali imekua haitoi kipaumbele kwa biashara za matandaonu lakini biashara za mtandaoni zinaweaza kuwa chanzo kikubwa cha mapato ya nchi na ajira kwa vijana. Mfano biashara ya kubadilisha fedha mtandaoni (FOREX) biashara hii haifaamiki na haijapewa idhini na serikali kutumika kama biashara nyingine za mitandaoni, Lakini biashara hii imekua ni chanzo kikubwa cha mapato na ajira kwa vijana hasa mataifa mengi ya ulaya na baadhi ya nchi za Afrika kama South Afrika na Kenya. Ombi langu kwa serikali itoe kipaumbele kwa biashara za mandaoni pamoja na kupunguza masharti magumu kwa watu wanao endesha baadhi ya biashara ya mtandaoni kama yuotube na blogs
Afya
Tumekua tukitumia pesa nyingi kununua madawa lakini baadhi ya madawa yamekua ni chanzo kikuwa cha magonjwa, Mfano tunanunua mbolea zenye kemikali kwa ajiri ya kilimo lakini baadhi kemikali zinabaki kwenye mazao ambayo baadae tunakuja kuyatumia kama chakula, Chakula ambacho ndani yake kina chembechembe za kemikali ambazo baadae zinakua chanzo cha magonjwa ambayo tuaagiza dawa ili tujitibu. Kama serikali itahimiza kilimo cha asili tutaweza kuimalisha afya zetu pamoja na kujikinga na magonjwa mengi.
Maendeleo ya Jamii
Maendeleo ni watu na watu wakiendelea na jamii huendelea pia. Serikali inabidi ipunguze kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo na badala yake itumie fedha hizo kuajiri vijana wanaomaliza vyuo na taasisi mbalimbali hii itasaidia kupunguza ongezeko kubwa la vijana wasiokua na kazi/ajira , kupunuza umasikini na kuongeza mzunguko wa fedha. Ili jamii iendelee lazima watu wake waendelee na kama seikali itatoa ajira nyingi kwa vijana iatachochea maendeleo kwenye jamii zao.
Utawala bora na Uwajibikaji
Ili tuwe na utawala bora lazima tuwe na usawa baina ya serikali na wananchi, Serikali isiwe juu ya wananchi ifikie kipindi ionekane inawanyonya na kuwakandamiza wananchi lakini pia wananchi wasiwe juu ya serikali mpaka ifikie kipindi serikali ionekane ni dhaifu. Ni lazima tuweke usawa baina ya serikali na wananchi ili tuwe na utawala bora
Upande wa uwajibikaji lazima kuwepo na mipaka ya madaraka yenye usawa, haki na sheria baina ya serikali na wananchi, Serikali isivuke mipaka yake na ikivuka iwajibishwe na wananchi ewasivuke mipaka yao na wakivuka waajibishwe.
Demokrasia
Hakuna demokrasia bora inayo toa haki na usawa kwa wananchi kwa asilimia 100 lakini zipo zenye unafuu. Mfano demokrasia ya moja kwa moja hutoa haki kwa wananchi kufanya maamuzi mfano sheria mpya iliyo tungwa. Nchi ya tanzania ipo kwenye mfumo wa demokrasia shirikishi ambao hautoi haki kwa wanachi kufanya maamuzi na badala yake hufanya na wawakilishi walioteuliwa na wananchi. Kumekua na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya sheria mpya zinazo tungwa na kupitishwa na bunge, Mfumo wa demokrasia ya moja kwa moja utamaliza malalamiko haya kwani wananchi watapata nafasi ya kufanya maamuzi juu ya sheria mpya. Serikali ijalibu kuuchunguza mfumo huu binafsi nauona ni mzuri.
Kilimo
Upande wa kilimo niishauri serikali itengeneze mahusiano chanya baina ya wakulima na wanunuzi kupitia bodi mbalimbali ilizo zianzisha . Mfano wakulima wapewe nafasi ya kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na wanunuzi, Bodi ziwepo lakini kwa ajiri ya kusimamia na kulinda haki za wakulima na sio kuwapangia bei elekezi tu na namna ya kuuza mazao yao
Sayansi na Teknolojia
Mfumo dhaifu wa elimu umekua ukichangia kuzolota kwa sayansi na teknolojia nchini kwetu. Kwa mfano serikali imekua ikitoa elimu ya nadharia kwa asilimia kubwa kuliko elimu ya vitendo Kuanzia shule za msingi hadi sekondari wanafunzi wanafundishwa nadharia kwa asilimia 80 na vitendo kwa asilimia 20 tu na hii imekua sababu kubwa kwa kuzolota michepuo ya sayansi ambayo huwaanda wanafunzi kuwa wanasayansi. Rai yangu kwa serikali ibadilishe mfumo wa elimu ianze kutoa elimu ya vitendo kwa alimia kubwa kuliko elimu yanadharia.
Haki za Binadamu
Watu wengi wamekua wakikosa haki zao kutokana na mifumo inayotumika. Mfano mfumo wa upelelezi, Mtu anakamtu akituhumia kwa makosa mbalimbali anapelekwa gerezani anakaa gerezani kama mahabusu kwa mda mrefu akisubili upelelezi kukamilika kisha anapelekwa mahakamani. Hii ni kinyume na haki za binadamu kwani watuhumiwa wengi wamekua wakikaa magerezani wakisubili upelelezi ukamilike na ukikamilika wanaonekana hawana wakosa. Serikali iangalie namna yakua inafanya upelelezi kwanza kabla ya kuwakamata watu hii itasaidia kupunguza idadi kubwa ya watu wanaokaa mahabusu wakisubili upelelezi kukamilika na mwisho wanakuja kuonekana hawana makosa.
Mwisho

Upvote
0