Rai Yangu kwa Usalama Wa Taifa

Rai Yangu kwa Usalama Wa Taifa

Maslahi ya Taifa ni mapana sana! Tathimini makini inahitajika kujua nini maana ya Maslahi ya Taifa.
"Heri punda afe lakini mzigo ufike"
Maslahi ya Taifa ni Maslahi ya wengi; Approach ya mgomo kudai maslahi ya madaktari wachache huku wengi wakiumia tena maskini na wengine wakifa haikuwa sahihi, kama ni wao wametumia njia hiyo kutuliza huo mgomo labla kuna maslahi ya wengi ambayo ndio ya Taifa kwa wakati huo.
 
Nini vision yao baada ya kuanzishwa kwa siasa ya vyama vingi? Siku zote dira ndio inakuwa chachu ya utekelezaji wa majukumu ya institution yoyote ile. naamini hawakujipanga vizuri baada ya kuisha kwa vita baridi juu ya nini idara hiyo ijikite zaidi kufanya zaidi ya kujitumbukiza kwenye siasa hizi za maji taka tena kwa lengo la kuhakikisha chama tawala hakitoki madarakani.

As we evolve as a nation, mambo mengi yanabadilika ila wao wako kama vile majuzi na jana. Ndio maana wanajikuta wanawekwa waziwazi kwenye mambo ambayo yanapoteza credibility ya chombo ambacho ni muhimu sana kwa uwepo na ustawi wa Taifa hili.

Tukumbuke wenzetu wanawatumia sana hawa jamaa for security and political gains in the time when globally, economic espionage comes first.Tunajisikiaje kuona matoke yanayolimwa Bukoba yanauzwa kwenye masoko ya dunia kutokea Kenya? Tunajisikiaje Tanzanite ya Tanzania inauzwa kwenye masoko ya dunia kutokea South Africa? Tunajisikiaje kuona mazao yanaoza mashambani ilhali kuna watu wanahaha kutafuta yanapatikana wapi? Tunajisikiaje tunapokuwa soko la bidhaa zisizo na viwango toka sehemu mbalimbali za ulimwengu huu?

It tells us we have stationed wrong people in various parts of the world. Pengine sasa idara ijipambanue kama idara na ichukue role yake inayostahili. Tunahitaji sana kuwa na idara makini, yenye tija na uwezo wa kuwa jicho la Taifa la Tanzania. Bila usalama wa Taifa kuwa imara, we are all in shit!
 
Shida kubwa tunayokuwa nayo katika nchi yetu ni kukiuka maadili ya wajibu wetu, badala ya kutimiza wajibu wao wa kikatiba, watu hawa wamejiruhusu kutawaliwa na kuongozwa na wanasiasa ambao wanaipeleka pabaya nchi yetu. Enzi za Mwalimu, usalama wa Taifa wala haukuwa usalama kwa wanasiasa!!!
 
Maslahi ya Taifa ni mapana sana! Tathimini makini inahitajika kujua nini maana ya Maslahi ya Taifa.
"Heri punda afe lakini mzigo ufike"
Maslahi ya Taifa ni Maslahi ya wengi; Approach ya mgomo kudai maslahi ya madaktari wachache huku wengi wakiumia tena maskini na wengine wakifa haikuwa sahihi, kama ni wao wametumia njia hiyo kutuliza huo mgomo labla kuna maslahi ya wengi ambayo ndio ya Taifa kwa wakati huo.


hakika umenena maslahi ya taifa ni maslahi ya wengi.

kama watu wengi wangeendelea kufa kwa mgomo wa madaktari wachache hakuna mantiki.

wengi walikuwa ni watanzania ambao wangeathirika na mgomo.
 
kubwa linaloonekana hapa ni kwamba analosema Dk. Slaa ndio final na ukweli mtupu hakuna kupinga.

Lakini Dk. anaweza kuwa anatumia mbinu ya mshambulie adui kabla hajakushambulia...... Dk. anawasakama hawa jamaa ili wasije wakatumika vibaya..... anawatangulia mbele na pengine ni mbinu za kisiasa kuelekea kuitwaa nchi.
 
Mawazo ni mazuri sana, lakini hao unaowaambia sasa, mh!

"checkup the real situation, nobody can stop them now! TOTAL DISTRUCTION THE ONLY SOLUTION" by Bob Marley

jamani eeh 2015 kama vp twende road tukomboe nchi yetu aliotugei Sir God hao hawackii ata mfanyaje zaid riz1 atazid tu kujenga majumba na kufungua sheli za mafuta kila kukicha nchi nzima!
 
ni vigumu kwa kuwa they are trained and paid for the purpose of sabotaging any one against the ruling class.

Pamoja na hayo sawa, lakini wakati wa nyerere waliibua maovu mengi sana na walikuwa na hadhi sana huwezi ukalinganisha na sasa hivi.Kipindi kile walijali maslahi ya Taifa.Hebu soma paragraph ya mwisho ya mtoa mada,utaelewa na maanisha nini.
 
kila taasisi ya nchi hii ilianza kuharibikiwa, kwa njia moja au nyingine, pale mkapa aliposhika hatamu. Jamani, tusiingalie tulipoangukia bali tulipo jikwaa.
Mwaswali ya msingi:

1. Nani alianza kuuza nchi? [nbc, ttcl, trc, atc, tanzanite, dhahabu, gesi,tanesco, mbuga za wanyama, lake victoria, msitu wa sao hill, kiwanda cha mgololo, kiwila, bandari, nyumba za serikali, tanesco, mbuga za wanyama, viwanda vya sukari e.tc.]

2. Nani aliasisi ufisadi wa kutisha? Meremeta, twine-tower, ndege, rada, epa, n.k........ Hivi unajua kuwa kabla ya ufisadi huu maximum wizi ndani ya serikali uliokuwa mkubwa sana ulikuwa around shilingi milioni mia mbili ama mia tano?

3. Nani alitukuza mfumo wa kukanyaga haki za watu kuishi, jeuri, ubabe, kiburi, na umungu-mtu?

4. Nani aliruhusu/alisaidia kuundwa kwa mtandao na hata ukasambaa kwenye asasi nyeti za umma?

Kwa taarifa yako kati ya laana mbaya kuwahi kuuipata nchi hii ni kuwepo kwa mtandao. Ilikuwaje kukawepo na kundi lenye madaraka na nguvu nje ya mfumo halisi wa madaraka?

Hayo yote niliyoyaanisha pale juu yasingeweza fanikiwa bila kwanza kuvuruga/kuharibu moral fabrics za hiki kinachoitwa "uwt". Uwt ndio msingi wa controls zote za serikali, sasa ukisha chakachua maadili na weledi wa idara hii unabakiza nini ktk taifa?
 
Hapo ndio wanapokosa muelekeo, wanageuka asasi ya chama tawala
ERnesto Che,
Kwani hujui kuwa ndani ya Usalama wa Taifa kuna Kitengo cha Kudhibiti CHADEMA na Wanaharakati? Je wategemea matokeo gani ktk Taasisi yenye Mrengo huo?
 
Angalia kazi za cia! Ni kusimamia chama tawala? Je ni kuua watu? Au ni kuua waanzisha midomo? Hujui unasema nn!
 
kila taasisi ya nchi hii ilianza kuharibikiwa, kwa njia moja au nyingine, pale mkapa aliposhika hatamu. Jamani, tusiingalie tulipoangukia bali tulipo jikwaa.
Mwaswali ya msingi:

1. Nani alianza kuuza nchi? [nbc, ttcl, trc, atc, tanzanite, dhahabu, gesi,tanesco, mbuga za wanyama, lake victoria, msitu wa sao hill, kiwanda cha mgololo, kiwila, bandari, nyumba za serikali, tanesco, mbuga za wanyama, viwanda vya sukari e.tc.]

2. Nani aliasisi ufisadi wa kutisha? Meremeta, twine-tower, ndege, rada, epa, n.k........ Hivi unajua kuwa kabla ya ufisadi huu maximum wizi ndani ya serikali uliokuwa mkubwa sana ulikuwa around shilingi milioni mia mbili ama mia tano?

3. Nani alitukuza mfumo wa kukanyaga haki za watu kuishi, jeuri, ubabe, kiburi, na umungu-mtu?

4. Nani aliruhusu/alisaidia kuundwa kwa mtandao na hata ukasambaa kwenye asasi nyeti za umma?

Kwa taarifa yako kati ya laana mbaya kuwahi kuuipata nchi hii ni kuwepo kwa mtandao. Ilikuwaje kukawepo na kundi lenye madaraka na nguvu nje ya mfumo halisi wa madaraka?

Hayo yote niliyoyaanisha pale juu yasingeweza fanikiwa bila kwanza kuvuruga/kuharibu moral fabrics za hiki kinachoitwa "uwt". Uwt ndio msingi wa controls zote za serikali, sasa ukisha chakachua maadili na weledi wa idara hii unabakiza nini ktk taifa?
 
Those in the intelligence dormain must be familiar with this tactic
 
There is always a man behind any tool, machine and system failure
 
Leadership is a like a machine or system.

To achieve the maximum efficiency and effectiveness, a machine or system requires a good design. The design stage is so critical such that an error or weakness at this stage is bound to severely impact the performance of the machine or system and eventually lead to failure.

However, sometimes we get past this hurdle and build ideal machines or systems. But due to bad or weakness in operations, they become less and less efficient and eventually fail.

No matter how good are systems or machines, if the operational culture and quality of people running them is poor, then failure and disfunction is imminent.
 
It takes twice as many crew (less than 27) to operate a supertanker(450,000DWT) as to

operate a dhow (450DWT)across the indian ocean. Despite the shear size of such a vessel

it is manned by few people, demonstrating the high level of efficiency and organisation.

Tanzania isnt too big to make it difficult for intelligence to function effectively and efficiently.
 
The failure we are witnessing

The dissfuction we are experiencing

is mere evidence that we have a PEOPLE issue/crisis.
 
Wadau.
NIMEKAA nikitafakari utendaji wa idara yetu ya Usalama wa Taifa. Hii ni taasisi muhimu sana kwa usalama wa nchi na wananchi wake, nchi zote idara hii ina heshima kubwa ndani ya jamii.
Kwa miaka mingi tangu uhuru wan chi yetu imekuwa na taasisi ya Usalama wa Taifa iliyo imara. Japokuwa mengi mabaya yalifanywa kipindi hicho na idara hii, lakini muktadha wangu naujenga kuhusu Hadhi na Heshima ya idara hii nyeti.
Hivi karibuni Usalama wa Taifa (idara) imeingia katika misukosuko kadhaa na wananchi wakiwemo wanasiasa. Mifano michache ni:

  1. Mwaka 2010 baada ya uchaguzi, aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema Dr Slaa alitoa shutuma za waziwazi kwa idara ya Usalama wa Taifa kuhusu kuhusika na wizi wa kura na kuingilia mchakato mzima wa uchaguzi ili kuipendelea CCM. Siku chache baadae Afisa mmoja wa Usalama wa Taifa alitoa taarifa kwa vyombo vya habari AKIKANUSHA.
  2. Tukio la Dr ulimboka limeiingiza idara ya Usalama wa Taifa tena ikiwataja moja kwa moja maafisa wake kutoka Ikulu, hakuna maelezo ya kutoka toka Ikulu kwenye hili
  3. Mbunge wa chadema (aliyevuliwa) Mh. Godbless Lema alitoa tuhuma kwamba hukumu ya kumvua ubunge ilitokana na maagizo ya Ikulu (Usalama wa Taifa ndio wahusika)
  4. Dr Slaa/ Mnyika wametoa shutuma za waziwazi wakiwataja maafisa wa Usalama wa Taifa kutaka kuwadhuru kwa staili mbalimbali

Hoja yangu
Idara hii ni muhimu sana, tena yenye heshima na hadhi kwa jamii, ifanye kazi ya kuhakikisha nchi iko salama ili matukio yanayoonyesha udaifu wa mfumo wa kuilinda nchi yetu yasitokee. Mfano Waethiopia wanavuka mpaka na kufia Dodoma katikati ya nchi, je wangekuwa maadui nchi ingesalimika? Je meli zetu zinapata ajali kila mara hakuna hujuma? Madini yanaibiwa na wahujumu uchumi wao wanafanya nini?
Rai yangu kwa usalama wa taifa ni kutoa kipaumbele maslahi ya Taifa sio kulenga kuwaua viongozi wa upinzani (kama kweli madai ya Dr Slaa)
Inasikitisha sana kuona taasisi hii muhimu kabisa kwa maisha na usitawi wa nchi yetu imechakachuliwa na kuwa kama ilivyo! Hili ni fundisho kwetu kwamba tunahitaji katiba itakayolinda na kutetea hadhi ya asasi nyeti kama hizi.

Serikali mbovu, legelege na ya kifisadi imeifikisha asasi hii hapa ilipo; haiingii kabisa akilini kuona watendaji serikalini wakisaini mikataba hatari kabisa kwa afya ya uchumi wanchi yetu mikataba iliyosainiwa na watu wenye elimu bora kabisa walioridhia vipengele ambavyo hata mwanafunzi wa cheti cha sheria angegundua kasoro zilizokuwemo! Mikataba hiyo ilipitishwa hata baada ya kuonwa na Usalama wa Taifa; - jicho la umma wa watanzania na asasi iliyotazamiwa kulinda maslahi ya nchi!

Tena haiingii akilini kabisa kuona genge la watu wakivamia Benki Kuu kupoora fedha kufanikisha kuchaguliwa waiongoze nchi; tena Usalama wa Taifa ukiwepo bila hata ya kuchukua hatua! Wakati wa uchaguzi usalama wa taifa wameshiriki ki uwaziwazi kuuhujumu kwa magari yao kutumika na chama tawala kufanyia kampeni, kuhujumu matokeo na sasa kuhusishwa na hujuma dhidi ya wananchi kama pale ilipogundulika baadhi ya wabunge (Wawakilishi wa wananchi) kutegewa vifaa vya kijasusi (na kudhuru afya zao labda), kujeruhiwa kwa silaha wabunge, kuuwawa wapinzani na hata kutekwa nyara na kuhujumiwa wanaharakati!

Ni wazi uharibifu ndani ya asasi hizi nyeti ni mkubwa kiasi cha kuhitaji matengenezo makubwa kabisa ambayo kwa hali ilivyo serikali hii haiyawezi labda ikija serikali nyingine itakayoanza kuzijenga asasi hizi upya kabisa. Mungu ibariki Tanzania.
 
No comments, tutayaona mengi.

Karl Marx once said, the ideas of the ruling class (government) are the ruling ideas.

That is what is happening at the moment.

Open your eyes and ears
 
Mawazo ni mazuri lakini pengine jambo la kuzingatia hapa ni nini hasa maana ya usalama wa taifa kwa mujibu wa taasisi hiyo nyeti; nijuavyo mimi kazi ya idara ya usalama wa taifa hasa ni kuhakikisha usalama wa serikali iliyoko madarakani na sivinginevyo. Muono wangu huo unaweza ukawashutua baadhi ya wana-JF lakini ndiyo hali halisi. Dhana hii ya usalama wa taifa inalandana na dhana ya maslahi ya umma, ambayo nayo pia inampa rais aliyoko madarakani turufu ya kuamua ni mambo yapi yapewe hadhi ya kuwa ni maslahi ya umma

Rais ni binadamu kama wengine.
Ana uzuri wake na mapungufu yake kama binadamu wengine.
Tusipoangalia, hata maslai yake binafsi anaweza kuyafanya yakaonekana kama ni ya Taifa!
Mengi yamefanyika kwa mgongo wa maslai ya Taifa.
 
Suala la chama kimoja cha siasa kukaa muda mrefu madarakani ndo madhara yake haya. matokeo yake inaonekana kama chama cha siasa ndio taifa lenyewe, kwa hiyo kwa wanausalama wetu, ukizungumzia usalama wa taifa unazungumzia usalama wa chama cha siasa kilichoko madarakani.
 
Back
Top Bottom