Unaweza kumwita kwa majina utakayo: rais wa ombaomba, nguli wa kuomba, mtoto wa mjini na mengineye.
Hata hivyo, unaweza kumwita mwamba aliyefikia hatua yakutunishiana misuli na mamlaka
unamkumbuka ombaomba huyu maarufu nchini? Alijulikana kwa jina moja la Matonya. Jina lake likawa kiwakilishi na msemo unawakilisha watu wanaoomba msaada wa fedha kwa jamaa, maratiki, au ndugu.
Ukiwa mtu wa kupenda 'kupiga mizinga' jina lililosadifu kwakolilikuwa matonya.
Matonya, ambaye jina lake halisi ni David Paulo, alizaliwa Kijiji cha Mpamatwa, wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Safari yake ya maisha mjini ilianza mwaka 1961 alipohamia Dar es Salaam kwa mara ya kwanza kwa kazi ya kuomba.
Matonya pia aliingia katika vuta nikuvute na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuf Makamba, alipokataa kurudi kijijini kwao Bahi.