Raia anapoonewa na Polisi anaweza kuishtaki Polisi?

Raia anapoonewa na Polisi anaweza kuishtaki Polisi?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kwa mfano mtu amekutana na OCD au RPC na huyo OCD au RPC akamtukana ama kumshambulia, jee raia huyo anatakiwa afanye nini ili aweze kumshtaki huyo OCD au RPC? Na jee RPC atashtakiwa kama mtu binafsi ama kama Polisi?

Jee Polisi wakivamia mahali kinyume cha sheria na kuanza kupiga watu bila ya sababu, jee polisi hao wanaweza kushtakiwa na mlolongo wa kuwashtaki unaanzia wapi?

Jee Wakuu wa Wilaya na Mikoa wanayo mamlaka ya kuwaamrisha Polisi kufanya kazi za upolisi kwa mujibu wa sheria. Jee maagizo yao yakileta madhara wanaoshtakiwa ni Polisi ama ni Wakuu wa Wilaya na Mikoa.
 
Kumshtaki inawezekana "No one is above the law",
Ila kupambana na hiyo kesi ndio mziki. Hakikisha vielelezo na ushahidi viko vizuri.
 
Pole kama mtoa hoja umefikwa na haya,hili ndilo tatizo la kuishi ndani ya shithole country,nchi zinazojielewa waliliona hili na ndio maana wana kitngo maalum chenye mamlaka kisheria wa kudeal na issue kama hii,yaani ni polisi wa kuona polisi wanafanya kazi zao kisheria(IPAD),au kijeshi ni kama MPs.tuendelee kusubiri tunaishi kwenye nchi yenye miungu watu wengi tu,tunawaogopa wanasiasa,wanajeshi,polisi etc etc
 
Inawezekana kikubwa isiwe ni majungu au mmegonganishwa huko guest.

Daima haki ina asili ya weupe.ukionewa ukakaa kimya hata mawe yatasimama kukupigania.
 
Kwa mfano mtu amekutana na OCD au RPC na huyo OCD au RPC akamtukana ama kumshambulia, jee raia huyo anatakiwa afanye nini ili aweze kumshtaki huyo OCD au RPC? Na jee RPC atashtakiwa kama mtu binafsi ama kama Polisi?

Jee Polisi wakivamia mahali kinyume cha sheria na kuanza kupiga watu bila ya sababu, jee polisi hao wanaweza kushtakiwa na mlolongo wa kuwashtaki unaanzia wapi?

Jee Wakuu wa Wilaya na Mikoa wanayo mamlaka ya kuwaamrisha Polisi kufanya kazi za upolisi kwa mujibu wa sheria. Jee maagizo yao yakileta madhara wanaoshtakiwa ni Polisi ama ni Wakuu wa Wilaya na Mikoa.

Maswali yako ni mengi mno...
 
Back
Top Bottom