Raia atakayetoa taarifa ya mhalifu Dar kulipwa Mil. 2

Wanakuuza mchana kweupe
 
Mshahara wa huyo kamanda ni bei gani ili nijue kama kweli ntapewa 2M au tutagawana na kikosi kazi 😅😅😅
 
Polisi wa bongo hawaaminiki
Umtaje askari ni mwalifu unajipenda kweli wewe 😂😂😂
Unaenda polisi kutoa taarifa. Halafu polisi hao hao wanawaambia wahalifu, kuna jamaa hapa anawajua vizuri shughuli zenu mmalizeni.

Wahalifu utawajua tu jinsi wanavyowakatisha tamaa raia wema. Ila kumbukeni kwamba hii ni ajira kama ajira zingine. Kisayansi inaitwa fursa kwenye changamoto.
 
WAfungue uzi hapa hapa JF watapata taarifa bila hata hayo malipo.
 
Wahalifu utawajua tu jinsi wanavyowakatisha tamaa raia wema. Ila kumbukeni kwamba hii ni ajira kama ajira zingine. Kisayansi inaitwa fursa kwenye changamoto.
Mkuu, kwanini kuandikia mate.

Wewe ukiokota kifaa chochote cha kijeshi au hata bunduki ipeleke polisi kwa nia njema tu.

Au ukikuta mtu kauawa, ametupwa wewe katoe taarifa polisi kwa nia njema tu.

Ukimaliza waulize wale wazee wa kufichua wakwepa kodi, kile kimgawo chao wanachoahidiwa na TRA huwa wanapewa ??!
 
Hela zinavyosumbua ,hili deal litapata wateja.Waandae tuu hizo chenji.Kwa sababu kuna kutoana sadaka majambazi kwa majambazi wao kwa wao.

Sema angetuambia hapa namna ya kutoa hizo taarifa,kumkopi IGP
 
Woga wako ndilo kaburi lako.

 
Mchezo Ukikamilika ?, Anyways ni Jambo Jema..., Ninashauri na fungu la hizi milioni mbili mbili zitoke kwenye yale makusanyo ya Faini kutoka kwa waharifu wengine
 
Serikali imebuni chanzo kipya cha ajira.

Sasa mimi kumpoint Dullayo Rasta na Side Nyenje ni kazi? Na hivi muda wote wanatembea na visu.

Narudi Dar kujiajiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…