Raia atakayetoa taarifa ya mhalifu Dar kulipwa Mil. 2

Polisi kwanza wawakamete askari wote wa Trafic wala rushwa ndio nitawaamini
 
Mbona hamjaandika kama ameua tena huyu jamaa? Tangia amehamia dar keshaua raia 6 akiwatoa kafara ili aonekane anafanya kazi, nitumie jukwaa hili kumpelekea ujumbe kwamba kila anayeua haishi muda mrefu ajikumbushe bwana shana yuko wapi aliyekuwa anaua watoto wa watu kisha anashangiria.

Muriro atambue kwamba polisi mwenye weledi haui watu anakamata baada ya kupeleleza na kwa kufanya hivyo anamaliza mtandao mzima was wezi/ majambazi.

Swali kwake ni je Mambosasa ambaye ameua mwishoni mwishoni kabla hajahamishwa hakuwa anayaona haya majambazi? Je rais Samiah anatamani kusikia mnaua raia wake kwa kutowapa nafasi ya kusema ukweli jinsi mlivyo na majambazi ndani yenu na wanawanufaisha?
ACHA MARA MOJA KUUA WATANZANIA!!
 
Mshahara wa constable tu haufiki million 2
 
Ila huyu RPC mpya inaonesha hatanii mtu
Ni RPC poa sana. Sisi wa Mwanza tumehuzunika sana kwa kuhama,lakini ndio sifa ya mwajiriwa. Ila kwenye hili la kutoa m. 2 eti kwa mtoa taarifa, HAPANA! Au nasema uongo ndugu zangu!!!???
 
Polisi wanazingua, kazi 8mewashinda wanataka kutumia pesa ya kodi zetu hovyo. Mbona miezi michache tu iliyopita hakukuwa na ahadi hizi za hela na ujambazi waliudhibiti kama sio kuukomesha? Imekuwaje sasa, au wameishiwa mbinu?


Vv
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…