Raia Ghana walalamika baada ya Rais wao Nana Akufo-addo kuzindua sanamu yake ilinokshiwa na rangi ya shaba!

Raia Ghana walalamika baada ya Rais wao Nana Akufo-addo kuzindua sanamu yake ilinokshiwa na rangi ya shaba!

Mbona Saddam alikuwa na Choo cha Solid Gold na mlikuwa mnamsifia.

Au umepata fursa tu ya kumkejeli Kiongozi Mweusi wa Kiafrika?!
Wananchi wake walikuwa wanaishije kwenye uongozi wake? Tuanzie hapo
 
Wananchi wake walikuwa wanaishije kwenye uongozi wake? Tuanzie hapo
Sunni Arabs walikuwa wanaishi vizuri na gerentii za kazi za Serikali kwa upande mwingine Shia Arabs walikuwa wakisakwa na vikosi vya Mukhabaraat vya Sadam na kubambikiwa kila aina ya makesi na kufungwa kupotezwa na kuuwawa.
 
Viongozi kama hawa ndiyo wanasababisha Trump na wazungu we wenzie wanatuzadharau ,inaaezekanaje Rais kujitengenezea sanamu ya mabilioni ili hali wananchi wake wengi wanaishi maisha mabovu???
 
Hawa
Marais wa Afrika ni walewale, uchawa na ujinga kila sehemu😹🤣🤣

====


Raia wa Ghana wametoa malalamiko yao baada ya Rais wa Nchini humo, Nana Akufo-Addo, kuzindua Sanamu yake iliyojengwa kwa kutumia Dhahabu katika Ukanda wa Magharibi mwa Nchi hiyo.​


Waziri Kwabena Okyere Darko-Mensah, amesema kuwa Sanamu hio imejengwa kwa Heshima ya Mipango na Maendeleo ambayo Rais amesimamia akiwa Madarakani. Ila kwa upande mwingine Waghana wamedhihaki Ujenzi huo wa Sanamu huku wakisema ni namna "Kujitukuza"​

Akufo-Addo, ambaye atang'atuka Madarakani Januari baada ya Mihula miwili Madarakani, amejigamba kuwa ametimiza asilimia 80 ya Ahadi zake kwa Waghana.​

 
Back
Top Bottom