Elections 2010 Raia Mwema: Dk Slaa awataka Duni, Hamad wa CUF

..kama CUF wako tayari kuunda mseto na CCM huko Zenj, sioni kwanini washindwe kuunganisha nguvu zao na Chadema huku Bara.
 

CUF kina nguvu Pemba tu. CHADEMA inakubalika sehemu kubwa ya jamhuri ya Tanzania ukiacha PEMBA. Sasa hapo chama kipi kinaheshimika zaidi? Wabunge wa CHADEMA wanaongoza kwa kuchangia kikamilifu bungeni. CUF inamtegemea Hamad rashid
 
Mnakubaliana na sisi kuwa chadema wamekurupuka, na wanaendelea kukurupuka kama tetesi hizi ni kweli, wana mgombea ambeye angeuzika vyema kama chama kimejitayarisha na kujieneza vizuri...hapa wanachotaka kukifanya hakieleweki hasa hata kama Hamad Rashid akikubali kuwa mgombea mwenza CUF hawatokuwa tayari kumuunga mkono kwa kuwa wanamgombea wao tayari, na kwa Hamad Rashid kuliwacha jimbo la Wawi ni kuliko usaliti kwa wananchi wa Pemba.

Zaidi chadema mnanajionyesha kuwa ni chama kisichotimia kimkakati na kimbinu, chama cha namna kama hiyo huonekana kufanya mambo yake kwa kubahatisha huku kikiamini kuwa kinafanya kwa uhakika.

Awali niliwahi kusema kuwa iwapo chadema hawana mtu wa kugombea urais uchaguziwa mwaka huu basi wamuunge mkono Prof.Lipumba huku wao wakijipanga zaidi kwa uchaguzi wa 2015...kitendo cha kuhaha kutafuta mgombea mwenza kutoka CUF kinaonyesha udhaifu wao wa kujipanga na kuipa usahihi ile dhana ya mwanzo kuwa wangeliamua tu kumuunga mkono Prof.Lipumba tokea mwanzo.

Sasa waendelee kuota kwa kuwa si Hamad Rashid wala Juma Duni Haji atakayekubali kuuingizwa kwenye siasa za kukurupuka kwa kuwa wawili hawa kadiri ninanyowafahamu wamesha sacrify makubwa zaidi ya hayo kwa ajili ya kukijenga chama cha CUF mpaka hapa kilipo.
 
Mkuu hilo ni gere tu bado hujasema kinachokusumbua kwa Prof.Lipumba na Maalim Seif...hao wenu chadema wanaofanana na wao wapo wapi? kwanini sasa mnahaha kuwatafuta Duni na Hamad Rashid...ni mashuhuri au?
CUF haihitaji kuunganisha nguvu ya chama chochote kwa kuwa imetimia na imejieneza vya kutosha,ndiyo maana umeona tumesimamisha wagombea wanaouzika na kukubalika bara na visiwani katika nafasi zote za urais, kazi kwenu mnaojiuza kwa umaarufu wa magazetini!
Sasa kama ni hivyo chadema watafute huyo mgombea mwenza kutoka Zanzibar anayekubalika...au wewe nitajie kama unamjuwa...! kama kweli unavyosema ndivyo vipi chama kinakubalika halafu kina haha kutafuta mgombea mwenza?
 
Junius,

..nadhani combination ya Slaa na Juma Duni ni more potent zaidi ya Dr.Lipumba na Juma Duni.

..kwenye siasa you never say never. hata kama CUF wameshaamua kumsimamisha Dr.Lipumba they still have time kubadilisha uamuzi wao na kuunganisha nguvu zao na Chadema.

..huku Tanganyika ni tofauti kidogo na Zenj. kwa upande wa Zenj, CUF doesnt need any other party to win the general election, lakini kwa huku Tanganyika, CUF na Chadema need to join forces in order to defeat CCM.

..CUF lazima waelewe kwamba CCM-Tanganyika ndiyo inayowapa kiburi CCM-Zenj kuwafanyia CUF rafu za kisiasa ktk uchaguzi mkuu wa Zenj. Chadema nao mpaka sasa hivi hawana m-Zenj mwenye status na ushawishi wa kuipa uzito ticket yao ya Uraisi wa Jamhuri.

..binafsi naona kumejitokeza a WIN-WIN opportunity na CUF na Chadema wanapaswa kuichangamkia.

NB:

..Dr.Lipumba ameshajaribu kugombea Uraisi mara 3 na zote ameshindwa. tangu mwaka 2005 hajafanya jambo lolote lile lililobadilisha nafasi yake na muonekano wake wa kisiasa machoni mwa wa-Tanganyika. kwa mtizamo wangu nadhani ingefaa awaachie wenzake ktk upinzani nao wajaribu.
 
Hii habari imenikosha sana. Maana kama hili litatimia basi watakuwa wametimiza kiu yangu ya kuona CUF na CHADEMA wanaungana na Rashid Ahmad anakuwa mgombea mwenza. Nilileta thread kabisa ya kujadili hili na ninashukuru wengi wenu mliniunga mkono. Kwakweli hapo CCM wataisikia Ikulu bombani. Tumenyanyaswa vya kutosha, tumetukanwa vya kutosha, tumenyonywa vya kutosha na hatimaye utawala wa wananchi unarejea.
 
Hatutaki mabadiliko yaliyotoka kanisani yenye agenda ya kikanisa, tunataka mabadiliko yaliyotoka kwa wananchi yenye agenda ya kuhudumia wa Tanzania wa dini zote. na kuheshimu dini zote ..Padre kuwa rais ni BIG NO!
Mlamba makombo ya RA umekuja huku tena udini utakuua siku moja.
 
Gobret

utachoka ndugu yangu huyu jamaa Tumain si wa kuimbia nyimbo ki ivyo jibu lake linalomfaa ni moja tu kama alivyoambiwa na ZionTZ

Originally Posted by ZionTZ

wewe ni F.A.L.A!!
 
sio shehe bana, sheikh
Shehe mangungo hivi ofisi bado hazijafungwa tu au ile laptop uliyonunuliwa na Rostam uneshaanza kuitumia, hongera endelea kujipendekeza mwisho utapewa grid ya taifa maana waarabu si unajua tena hawacheleweshi.
 
Wote wanaopinga wazo la CUF na CHADEMA kuungana na wanaoleta kejeli za kidini ndiyo mafisadi, majizi, majambazi, vibaka na kila aina ya waovu wa nchi hii, ambao wanajua kuingia kwa upinzani madarakani utakuwa ni mwiba kwao na hakutakuwa na nafasi tena ya wao kula nchi wakati wengine wakiugua kwa kuijenga. Hivi inakuwaje mtanzania wa kawaida mwenye shida kama za sisi wengine ajiinue kwa mbwembwe kabisa kumponda Dr Slaa na mpango wa hivi vyama viwili kuungana ili kuing'oa CCM? Hivi ni Mtanzania gani, mvuja jasho wa kawaida anayeweza kusimama mbele za watu akiwa na akili timamu kabisa na kuanza kuisifia CCM na Kikwete kama siyo mla rushwa tu?
Tumain, MS na Junius, kama mnaona twawakela tuacheni tuendelee na mjadala wetu. Haisaidii kuja kutuvurugia mijadala yetu ya kujenga nchi yetu. Ninapenda kuwatahadharisha kwamba mmeshachelewa sana, tayari tushampitisha Dr Slaa kuwakomboa watanzania, kama Hamad Rashid atakubali or not hicho hakitakuwa kigezo cha sisi kurudi nyuma. Na isitoshe tunamtafuta Rais wa jamhuri ya Tanzania na si Rais wa Zanzibar, kwa hiyo anaweza kusimamishwa yeyote akagombea na Dr Slaa kwa maana hata asipate kura hata moja kutoka Zanzibar bado atakuwa ni Rais wa jamhuri ya muungano. Mtake msitake atakuwa Rais wenu. Tuacheni tujadili mambo ya maana hapa, msitake kutuvuruga na ufisadi wenu.
 

Mkuu hapa suala si kujenga chama, wanaweza kuangalia interests za taifa na si chama. Kama combinations zao zaweza kuleta ukombozi kwa taifa, kuna tatizo gani mmoja wao akashindwa kuwa mgombea mwenza?
 
ukiona hivi ujue ccm au mgombea wa ccm maji yako shingoni, hivyo kilicho baki ni kutumia bomu la nuklia ya kidini, na hiyo ccm kwa kuwa na mwelekeo kama huu time bomb, hiyo ndoa ya mafisadi karibu italipuka.
 
Wewe Tumain unangoja nini si uhame mbona wengi walifanya hivyo nyakati zileeeeee!!kama unaona Tz. ilikosewa tangu enzi za mchonga kinachokufanya ukose raha na watu na ni nini... Tanzania ni ya watu wote wa dini zote makabila yote na sisi kama watanzania tupo tayari kuongozwa na mtu wa dini yoyote,kabila lolote as long as yupo kwa manufaa ya watanzania wote period. Sasa sijui kipi kisichoeleweka hapa kwako.
 
Ni Profesa Lipumba....tena ni wa uchumi...si Dr....wa...!!!!
Hivi huyu king'ang'anizi wa madaraka ni babu yako au mjomba wako. Watu wanaokula makombo utawaona tu wanavyojitahidi kutetea upupu ilimradi tu yale mabaki yaliyokuwa yanadondokea karibu yao yasiondoke. We mtu kagombea 1995, hola, 2000 hola, 2005 kura ndo kwanza zikashuka kabisa. Wewe bado una imani tu kwamba sasa atashinda? Au ni zile mlizoamua kumnyima Kikwete kwa kuwalaghai kuhusu mahakama ya kadhi ndo mnafikiria kumpa Lipumba? My friend hebu nenda na wakati. Huyo Lipumba kama watu hawakumpa Urais mwaka 2000 alipopata support ya CHADEMA wala msitegemee kura zetu tena. Tunataka sura mpya. Si ajifunze kutoka kwa mwenzie Mbowe?
 

Mkuu kama unafikiri siasa ni sawa na mchezo wa mpira wa miguu unakosea, hebu soma kidogo taarifa za mtu huyu hapo chini:


kama ingelikuwa Wade ni kocha na timu anayofundisha ni Real Madrid ningekubaliana na wewe lakini mkuu hii ni siasa.
 
Brilliant ideas i.e. ku-join nguvu kati ya CHADEMA na CUF.............

Bandugu tuendelee kupiga kampeni kwa ndugu zetu jamaa na marafiki ili wamchague Dr. Slaa..........nimuhimu.....muda ni mfupi sana wa kufanya hizi kampeni
 
CUF mnashangaza: yaani chama chenu hakuna wanasiasa mashuhuri zaidi ya Profesa wenu wa Pumba na yule Maalim Seif.

Kaka kama una mengine ya kukosoa yatoe lakini sio kudhihaki USOMI wa hawa wazee wetu. Kama unabisha nenda Mlimani ukapate kujua record zao ndio uanze dhihaki zako. By the way mkiaanza kukashifu watu kuhusu usomi wao naamini upande wenu ndio upo more vulnerable kuliko CUF.

omarilyas
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…