Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yaani CHADEMA mnasikitisha sana sana ,nitaona ajabu kama badu kuna watu awajaistukia CHADEMA kuwa ni patupu ,nilitegemea mngetaka kuungwa mkono kumbe mnataka vigogo tena wakuu wa Chama cha Upinzani hapa Tanzania ,hivi akina LWAKATALE hakuwatosheni Shaibu Akwilombe mmempeleka wapi ????
Hivi huko hakuna watu wenye ushawishi ,nilitegemea mngehitaji CUF iwaunge mkono bila ya kuhitajia watu fulani ,? Hivi mnakumbuka kama mliungwa mkono kule Tarime na je mlipotakiwa muiunge mkono CUF pale Mbeya ,mlifanyaje ? Ni lini CHADEMA mlimuunga mkono CUF kupitia mgombea wake Lipumba ? Hivi ni akina nani wale waliojitoa katika dakika za mwisho ?
CUF ni chama chenye kuheshimika dunia nzima na hapa Tanzania amini usiamini bado ni Chama nambari moja katika kutoa upinzani mkali ,Chadema ndio mnahitajiwa kuiunga mkono CUF Chama kilichokamilika hakihitaji mtu kutoka sehemu yeyote ile.
Yaani tayari mmeonyesha kama mna kasoro tena kubwa sana ,au sijawaelewa ???
..kama CUF wako tayari kuunda mseto na CCM huko Zenj, sioni kwanini washindwe kuunganisha nguvu zao na Chadema huku Bara.
Mkuu hilo ni gere tu bado hujasema kinachokusumbua kwa Prof.Lipumba na Maalim Seif...hao wenu chadema wanaofanana na wao wapo wapi? kwanini sasa mnahaha kuwatafuta Duni na Hamad Rashid...ni mashuhuri au?CUF mnashangaza: yaani chama chenu hakuna wanasiasa mashuhuri zaidi ya Profesa wenu wa Pumba na yule Maalim? Ni hao hao tu wanakikaba koo chama chenu kwa miaka 20 sasa bila kufurukuta, na eti mnawaona wanafaa kila uchaguzi pamoja na kwamba wanalizwa kila uchaguzi? Ndo maana Lwakatare aliwakimbia.
CUF haihitaji kuunganisha nguvu ya chama chochote kwa kuwa imetimia na imejieneza vya kutosha,ndiyo maana umeona tumesimamisha wagombea wanaouzika na kukubalika bara na visiwani katika nafasi zote za urais, kazi kwenu mnaojiuza kwa umaarufu wa magazetini!..kama CUF wako tayari kuunda mseto na CCM huko Zenj, sioni kwanini washindwe kuunganisha nguvu zao na Chadema huku Bara.
Sasa kama ni hivyo chadema watafute huyo mgombea mwenza kutoka Zanzibar anayekubalika...au wewe nitajie kama unamjuwa...! kama kweli unavyosema ndivyo vipi chama kinakubalika halafu kina haha kutafuta mgombea mwenza?CUF kina nguvu Pemba tu. CHADEMA inakubalika sehemu kubwa ya jamhuri ya Tanzania ukiacha PEMBA. Sasa hapo chama kipi kinaheshimika zaidi? Wabunge wa CHADEMA wanaongoza kwa kuchangia kikamilifu bungeni. CUF inamtegemea Hamad rashid
Mlamba makombo ya RA umekuja huku tena udini utakuua siku moja.Hatutaki mabadiliko yaliyotoka kanisani yenye agenda ya kikanisa, tunataka mabadiliko yaliyotoka kwa wananchi yenye agenda ya kuhudumia wa Tanzania wa dini zote. na kuheshimu dini zote ..Padre kuwa rais ni BIG NO!
GobretTumain, nahisi kuwa umekosa matumaini ndio maana unajibu kama mtu aliyekata tamaa ya kuishi. Maisha ni mapambano na SIASA NI JUKUMU LETU SOTE: WAO, WEWE, MIMI, kila mtu. Usilete mchezo wala utani. Siasa hugharimu maisha ya watu wasio na hatia kama sasa Watanzania wanajutia kuipa CCM nchi na SASA WANAHAHA ISIKU NA MCHANA NJAA TUPU NA KUIONDOA MADARAKANI IMEKUWA KAZI KWELI KWELI. Dk Slaa unamwita padri asiyefaa kitu: HAYO NI MAONI YAKO. Hakuna anayejua unafaidika vipi na CCM. Pengine hata mimi kama sina utaifa na uzalendo wa kweli na ningekuwa nafaidika moja kwa moja na CCM ningekuwa nafanya kama wewe. Si kosa lako ni NJAA NA KUTOFAHAMU. Huna uchungu na hii nchi. Kama ungekuwa nao basi usingethubutu kuleta suala la kutugawa Watz kwa misingi ya imani na itikadi zetu. Binafsi: Ninamwangalia mtu wala si chama, kabila wala dini anakotoka. Awe padri, askofu, mchungaji, ustadhi,imamu kwangu si tatizo. Mchungaji Mama Rwakatare alipochaguliwa/teuliwa kuwa mbunge wa viti maalum, waliofanya hivyo walikuwa wakristu? Au madhehebu ya Kikristu? Bila shaka jibu ni HAPANA. HUU UDINI wako unautoa wapi? Tukiwa tunawachagua watu kwa dini zetu nani atakuwa raisi wa nchi? Na watu wa imani fulani wakishinda, wa imani nyingine watakwenda wapi? Jiulize nini HATMA ya nchi yetu. Unaporopoka uangalie heshima uliyonayo, UMRI ulionao na Picha unayoacha. God bless DK SLAA. GOD BLESS TANZANIA
Shehe mangungo hivi ofisi bado hazijafungwa tu au ile laptop uliyonunuliwa na Rostam uneshaanza kuitumia, hongera endelea kujipendekeza mwisho utapewa grid ya taifa maana waarabu si unajua tena hawacheleweshi.sio shehe bana, sheikh
Mnakubaliana na sisi kuwa chadema wamekurupuka, na wanaendelea kukurupuka kama tetesi hizi ni kweli, wana mgombea ambeye angeuzika vyema kama chama kimejitayarisha na kujieneza vizuri...hapa wanachotaka kukifanya hakieleweki hasa hata kama Hamad Rashid akikubali kuwa mgombea mwenza CUF hawatokuwa tayari kumuunga mkono kwa kuwa wanamgombea wao tayari, na kwa Hamad Rashid kuliwacha jimbo la Wawi ni kuliko usaliti kwa wananchi wa Pemba.
Zaidi chadema mnanajionyesha kuwa ni chama kisichotimia kimkakati na kimbinu, chama cha namna kama hiyo huonekana kufanya mambo yake kwa kubahatisha huku kikiamini kuwa kinafanya kwa uhakika.
Awali niliwahi kusema kuwa iwapo chadema hawana mtu wa kugombea urais uchaguziwa mwaka huu basi wamuunge mkono Prof.Lipumba huku wao wakijipanga zaidi kwa uchaguzi wa 2015...kitendo cha kuhaha kutafuta mgombea mwenza kutoka CUF kinaonyesha udhaifu wao wa kujipanga na kuipa usahihi ile dhana ya mwanzo kuwa wangeliamua tu kumuunga mkono Prof.Lipumba tokea mwanzo.
Sasa waendelee kuota kwa kuwa si Hamad Rashid wala Juma Duni Haji atakayekubali kuuingizwa kwenye siasa za kukurupuka kwa kuwa wawili hawa kadiri ninanyowafahamu wamesha sacrify makubwa zaidi ya hayo kwa ajili ya kukijenga chama cha CUF mpaka hapa kilipo.
ukiona hivi ujue ccm au mgombea wa ccm maji yako shingoni, hivyo kilicho baki ni kutumia bomu la nuklia ya kidini, na hiyo ccm kwa kuwa na mwelekeo kama huu time bomb, hiyo ndoa ya mafisadi karibu italipuka.Kama kuchafua ni kusema kweli na iwe hivyo...ya nini waanze kujuta kama wazee wetu....heri nusu shari kuliko shari kamili...hao cuf waendeleze chama chao cha wananchi ya nini kuungana na watu wanaofuata maagizo ya kanisa ndugu. nashauri tu wakitaka waende lakini watakuwa walewale watu wakujipendekeza halafu watatoswa na kutukanwa kama JK si alikuwa chaguo la mungu akajipendekeza sasa wamemtosa.
..Dr.Lipumba....
Hivi huyu king'ang'anizi wa madaraka ni babu yako au mjomba wako. Watu wanaokula makombo utawaona tu wanavyojitahidi kutetea upupu ilimradi tu yale mabaki yaliyokuwa yanadondokea karibu yao yasiondoke. We mtu kagombea 1995, hola, 2000 hola, 2005 kura ndo kwanza zikashuka kabisa. Wewe bado una imani tu kwamba sasa atashinda? Au ni zile mlizoamua kumnyima Kikwete kwa kuwalaghai kuhusu mahakama ya kadhi ndo mnafikiria kumpa Lipumba? My friend hebu nenda na wakati. Huyo Lipumba kama watu hawakumpa Urais mwaka 2000 alipopata support ya CHADEMA wala msitegemee kura zetu tena. Tunataka sura mpya. Si ajifunze kutoka kwa mwenzie Mbowe?Ni Profesa Lipumba....tena ni wa uchumi...si Dr....wa...!!!!
...We mtu kagombea 1995, hola, 2000 hola, 2005 kura ndo kwanza zikashuka kabisa. Wewe bado una imani tu kwamba sasa atashinda? Au ni zile mlizoamua kumnyima Kikwete kwa kuwalaghai kuhusu mahakama ya kadhi ndo mnafikiria kumpa Lipumba? My friend hebu nenda na wakati. Huyo Lipumba kama watu hawakumpa Urais mwaka 2000 alipopata support ya CHADEMA wala msitegemee kura zetu tena. Tunataka sura mpya. Si ajifunze kutoka kwa mwenzie Mbowe?
[Abdulaye Wade] A long-time opposition leader, he ran for President four times, beginning in 1978, before he was elected in 2000...
Wade first ran for Presiden t in February 1978 against Senghor, taking 17.38% of the vote. Senghor gave Wade the nickname "Diombor" (Wolof for hare). Also in 1978, Wade was elected to the National Assembly, where he served until 1980. Subsequently he ran in the presidential elections of 1983 and 1988, taking second place each time, behind Senghor's successor Abdou Diouf. Following the 1988 election, he was arrested due to protests against the results and received a suspended sentence. Subsequently he went to France, but returned in 1990...In the February 1993 presidential election, Wade again took second place, with 32% of the vote, behind Diouf, who won with 58%.... In the first round of the 2000 presidential election, held on February 27, he again took second place, receiving 31% of the vote, but for the first time, Diouf did not win a first round majority, and consequently a second round was held on March 19. Wade won this round with 58.49% of the vote...Wade became President on April 1, 2000 until to date....
source: wikipedia
CUF mnashangaza: yaani chama chenu hakuna wanasiasa mashuhuri zaidi ya Profesa wenu wa Pumba na yule Maalim Seif.