Raia Mwema: Tundu Lissu atoswa rasmi


Gazeti la Raia mwema kwani si ni la Ulimwengu, au ?
 
Lissu bado anaamini katika siasa za haki, wakati wenzake wanakenua Meno Kwa kuahidiwa kupewa majimbo 2025.

Chadema ya Mbowe sasa inasubiri kila kitu iambiwe toka Magogoni.
 
Acha kumfananisha Magufuli na ujinga wa MIGA na kuolewa Ubelgiji
 
Raia Mwema ndiyo limekuwa la.kisengerema hivi? Wajifunze kwa Tanzanite la Musiba. Inasikitisha sana gazer lilokuwa linaheshimika leo limekuwa la kipuuzi hivi.
Nyumbu wa walamba asali unapingana na habari ya gazeti ambayo Iko wazi
 
Gazeti limejitoa ufahamu?

Acha unyumbu
 
Hiyo 'lead story' mhu!
 
Namisi sana vipindi vya 'this week in perspective', malumbano ya hoja, kipima joto, jicho letu ndani ya habari, Mlimani TV etc vya enzi hizo.
 
Tatizo ni kuwa kila mtu anaangalia tumbo lake. Hii iaashiria kuwa hakutakuwa na Katiba Mpya hapa TZ kama hatutakuwa makini.

Katika chadema kuna makundi mawili
1. Ni akina Mbowe na Lema wake, wenyewe wanahangaika na UBUNGE. Hivyo Maridhianao yalikuwa Samia aachiwe Urais na wao waachiwe ubunge. Wakaona kila kitu safi ndiyo maana unasikia kila siku kumpamba Samia. Hata mabaya yanayoonekana kwa awamu ya 6 wao kimya. Kikibwa wamehaidiwa Ubunge (Nusu Mkate).
2. Tundu Lissu hataki ubunge bali URAIS tu. Hivyo yeye anaona hakuna haja ya kuhaidiwa ubunge bali kungekuwa na kuhaidiwa Urais, yeye kiu yake ingepona. Sasa wenzake wamemtupa maana alitegemea nusu nyingine ya mkate iwe Samia kumwambia Lissu kuwa nitakuachia kiti.

Huo ndiyo mgawanyiko wa Chadema ambao akina Erythrocyte , Retired Mmawia brazaj hawaelewi mambo. Wanaburizwa tu kwa maslahi ya wachache.

Je, kwa mwendo huu, kutapatikana Katiba isiyokuwa na maslahi binafsi?
 

Kwa akili ya kawaida tu ulitakiwa ujiulize ametoswa baada ya kikao gani, na ni kiongozi gani wa CDM ametoka hadharani kusema wamemtosa Lisu? Ifahamike hadi sasa Lisu yuko kwenye ziara za chama akifanya mikutano. Aliyetoswa anawezaje kuendelea kufanya mikutano ya chama? Kama ni mbinu ya gazeti kuuza hilo sio tatizo.
 

Hapa ndio unaona umecheza mind game ya hatari.
 
Raia Mwema ni mouthpiece ya ACT Wazalendo,na adui namba moja wa ACT Wazalendo ni Chadema.
 
Siamini chochote hapo mpaka nimsikie mwenyewe Mbowe akiyasema haya au Lissu
 
Badala ya kujibu hoja unajificha kwenye kichaka Cha Sukuma gang ?
Hakuna hoja ya kujibu hapo,hizo ni speculation za mwandishi ambaye ana chuki na Chadema. Ukweli uliowazi ni kuwa Chadema wako kitu kimoja na kwa vile wao siyo misukule wana mitazamo na maoni tofauti lakini wana lengo moja ndiyo maana viongozi wote wa juu wanaenda Kigoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…