Raia mwenye asili ya Congo apigwa na Polisi hadi kufa nchini India

Alvin_255

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2015
Posts
246
Reaction score
503
Mkongomani auwawa kwa kupigwa hadharani na Polisi nchini India. Kifo cha Mkongo huyo kimesababisha mandamano kwa raia walivyoona akipigwa marungu na miti kichwani na kiunoni kwa kushambuliwa na Polisi Zaidi ya 8 bila Huruma hadi alipokata roho na kuendelea kupiga maiti kwa kuiponda-ponda.



Wahindi nchini DRC, wanahofia maisha yao kutokana na hali ya hasira ilioanza kuonekana dhidi yao, kwenye nyuso za Wakongomani walio ndani na nje ya nchi, kufwatia kifo cha raia huyo aliyepoteza maisha akiwa mikononi mwa jeshi la Polisi nchini India.



Tukio ambalo limezuwa Hali ya sintofahamu na kusababisha maandamano na vurugu kufanyika ndani na nje ya nchi.
Kufikia sasa, Serikali za mataifa hayo mawili zimeingilia jambo hilo lenye utata na kuanza kujaribu kulitatuwa.

 
Mauji tena, tena kwa chombo cha dola? Taasisi ya kupeleka malalamiko ndio wana tu ua?, Hadharani kama umbwa. Alafu tunaangalia tu, tunayazungumza yanaisha. Dah! shame on us.
 
India wapuuzi sana.....tena police walioua wanaonekana kabisa watu wazima
 
Ila raia wa kikongo wakiuliwa na polisi wa Congo mambo ni mshwano kabisa?
Rejea kifo cha Akwelin na Mwangosi...double standard kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…