Mkongomani auwawa kwa kupigwa hadharani na Polisi nchini India. Kifo cha Mkongo huyo kimesababisha mandamano kwa raia walivyoona akipigwa marungu na miti kichwani na kiunoni kwa kushambuliwa na Polisi Zaidi ya 8 bila Huruma hadi alipokata roho na kuendelea kupiga maiti kwa kuiponda-ponda.
View attachment 1881981
View attachment 1881982
Wahindi nchini DRC, wanahofia maisha yao kutokana na hali ya hasira ilioanza kuonekana dhidi yao, kwenye nyuso za Wakongomani walio ndani na nje ya nchi, kufwatia kifo cha raia huyo aliyepoteza maisha akiwa mikononi mwa jeshi la Polisi nchini India.
View attachment 1881984
Tukio ambalo limezuwa Hali ya sintofahamu na kusababisha maandamano na vurugu kufanyika ndani na nje ya nchi.
Kufikia sasa, Serikali za mataifa hayo mawili zimeingilia jambo hilo lenye utata na kuanza kujaribu kulitatuwa.
View attachment 1881986