Raia wa Burundi Ashitakiwa kughushi Kitambulisho cha Mpiga kura na NIDA

Raia wa Burundi Ashitakiwa kughushi Kitambulisho cha Mpiga kura na NIDA

Kuna vijana wa nchi inayopakana na Burundi waliokuwa wanasoma UDSM walikuwa wananunua viwanja huko mkuranga miaka ya nyuma. Bila shaka wameshapoteana tangu mfumo wa NIDA uanze kazi. Hata hivyo serikali ifuatilie hayo maeneo ya mkuranga ihakiki viwanja vyote maana hata magaidi walikuwa kule. Kwahiyo hao raia wa nchi jirani wanatakiwa kuangaliwa kwa umakini sana maana wameshazoea machafuko kwenye nchi zao.
 
Raia wa Burundi, Kabura Kossan (65) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akikabiliwa na mashtaka sita yakiwemo ya kughushi kitambulisho cha Taifa (Nida) na cha Mpiga kura.

Vilevile anadaiwa kutakatisha Sh8 milioni zilizotokana na kununua eneo lene ukubwa wa heka 100 lililopo Kijiji cha Kibesa, Wilaya ya Mkuranga, huku akijua anaishi nchini Tanzania kinyume cha sheria.

Mshtakiwa huyo amesomewa mashtaka yake leo Jumanne, Agosti 27, 2024 na wakili wa Serikali, Aaron Titus, Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ushindi Swallo.

Hata hivyo, kabla ya kusomewa shtaka hilo Hakimu Swallo amesema mshtakiwa hatakiwi kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi.

Hakimu Swallo amesema mshtakiwa hatakiwi kujibu chochote kutokana shtaka la kutakatisha fedha kutokuwa na dhamana.

Akimsomea mashtaka hayo, wakili Titus amedai mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 24289/ 2024. Amedai katika shtaka la kwanza, Kossan anakabiliwa na shtaka la kuwepo nchini bila kuwa na kibali.

Anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 17, 2024 ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inadaiwa siku hiyo mshtakiwa akiwa raia wa Burundi, alikutwa akishi nchini bila kibali. Shtaka la pili, katika tarehe isiyofahamika ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mshtakiwa alighushi Kitambulisho cha Mpiga Kura chenye jina la Charles Ng'andu kwa lengo la kuonyesha kuwa kimetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Wakili Titus amedai shtaka la tatu ni kuwasilisha kitambulisho hicho cha kughushi cha Mpiga kura kwa
maofisa wa Polisi. Shitaka la nne, mshtakiwa huyo anadaiwa katika tarehe isiyofahamika, alighushi kitambulisho cha Taifa chenye jina la Charles Ng'andu akionyesha kuwa kimetolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Iliendelea kudaiwa kuwa mshtakiwa huyo baada ya kughushi Kitambulisho cha Nida, alikiwasilisha kwa maofisa wa Polisi, wakati akijuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria. Shtaka la sita ni kutakatisha fedha, tukio analodaiwa kulitenda kosa hilo Septemba 15, 2010 ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Inadaiwa siku hiyo ya tukio, mshtakiwa akiwa raia wa Burundi aliweza kujipatia eneo lenye ukubwa wa heka 100 lililopo kijiji cha Kibesa, Wilaya ya Mkuranga kwa gharama ya Sh8 milioni, huku akitambua kuwa fedha hizo ni mazalia ya kosa tangulizi la kuishi chini bila kuwa na kibali.

Upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na kwamba wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Swallo alisema shtaka la kutakatisha fedha linalomkabili mshtakiwa huyo, halina dhamana kwa mujibu wa sheria, hivyo ataendelea kukaa rumande hadi kesi yake itakapoisha.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Swallo aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 9, 2024 kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa alirudishwa rumande.

SOURCE: MWANANCHI​
Mbona wako wengi tu Morogoro sehemu inaitwa Lukobe, wamekuwa wakishushwa huko na treni za mizigo japo Zitto atabisha
 
Mbona wako wengi tu Morogoro sehemu inaitwa Lukobe, wamekuwa wakishushwa huko na treni za mizigo japo Zitto atabisha
Kweli mkuu wanajiita waha najiuliza mbona waha wanakuwa wengi sana morogoro
 
Wewe utakuwa hujasoma hiyo story vizuri?
Huyo mrundi ndio just amenunua hilo shamba .
Wabongo watakuwa wamemzunguka wamemtapeli na kumuangushia jumba bovu
Tangu Septemba 15, 2010
 
Eka 100 milion 8 afu raia wa burundi aloo achomoki, kuna vitu bana utadakwa tu, angeuza mapema akasepa zake kwao uko
Namjua.....

Ana Mke Tanzania.
Ana Watoto Tanzania.
Ana Wajukuu Tanzania.
Mtoto wake wa kwanza kazaliwa 1987....!!!t

Anaishi hapa toka miaka ya 1980 mwanzoni.



 
Namjua.....

Ana Mke Tanzania.
Ana Watoto Tanzania.
Ana Wajukuu Tanzania.
Mtoto wake wa kwanza kazaliwa 1987....!!!t

Anaishi hapa toka miaka ya 1980 mwanzoni.



Mahusiano na mkewe yakoje!? Isijekua mke ndiyo katoa taarifa za kiintelegensia kwa mamlaka!!?
 
Isije kua ni mgogoro wa Aridhi umezaa yote haya!!??
Kabisa maana haiingii akilini et amegushi,katakatisha fedha,kajipatia eneo....mpk anafikishwa mahakaman nn chanzo? Hii siyo bure Kuna jambo nyuma ya pazia
 
Yes, alinunua zamani Sana, na lilikua Pori tu, akafyeka na kuanza Kulima, Sasa Pori likawa Shamba, Watu wakaanza kulitamani Shamba lake.
Hapo sawa kabisa wew umeeleza vyema na hapo Kuna rushwa imetumika
 
Mahusiano na mkewe yakoje!? Isijekua mke ndiyo katoa taarifa za kiintelegensia kwa mamlaka!!?
Hapana, ni Watu wazima, wanaishi na Wajukuu zao, Wana Mahusiano mazuri tu na Mke wake.
 
Back
Top Bottom