Bogotá Colombia 13 OCT 2022
Dar es Salaam 13 Oct 2022
Raia wa Colombia hatimaye ataachiwa baada ya plea bargain US$ 25,000 baada ya kusota katika gereza jijini Dar es Salaam kwa miaka nane tangu mwezi Julai mwaka 2014 hadi mwezi October 2022.
Ndugu na jamaa zake waliendesha kampeni kubwa juu twitter juu ya 'kuonewa' kwa Andres Filipe Ballesteros kufunguliwa kesi asiyoijua, lakini upande wa kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya walikuwa na ushahidi wa kutosha usio na shaka kuhusu Andres Filipe Ballesteros.
Maandamano ya wabeba mapango nchini Colombia yakiichagiza serikali yao imuokoe kutoka gerezani Tanzania yalipamba moto na wizara husika nchini Colombia kuanza kuanzisha mazungumzo na ofisi ya mundesha mashtaka Tanzania ili kujua ukweli.
Maafisa wa wizara ya sheria Colombia waliweza kufungua channeli za kidiplomasia kuwasilisha US$25,000 sawa na TShs. 50,000,000 kwa vyombo vya sheria Tanzania kuwezesha kumtoa gerezani Andres Filipe Ballesteros arudi nyumbani kwao Colombia .
Andres Filipe Ballesteros Uribe alikamatwa mwaka 2014 nchini Tanzania ktk kiwanja cha ndege cha kimataifa cha JNIA jijini Dar es Salaam Tanzania akiwa ameficha madawa katika mvunguko wa suruali kiunoni na pia ktk mkanda aliovaa.
TOKA MAKTABA :
JULY 2014

Mkuu wa Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa akionesha Cocaine zilizokuwa zimefichwa katika mkanda wa suruali aliyokuwa amevaa raia wa Colombia, Andres Filipe Ballesteros Uribe (28), mara baada ya kukamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Alianza safari yake Julai 2014 nchini Columbia, kupitia Addis Ababa kuja Tanzania huku akibainisha kwamba hiyo ni njia mpya ya usafirishaji wa dawa hizo haramu.
“Hawa jamaa wanajaribu kubuni mbinu mpya kama huyu kijana alikuwa amefunga unga wa cocaine kama zilivyokuwa zikifungwa pipi na akazimeza… mpaka sasa ameshatoa pipi 13 kwa njia ya haja kubwa na anaendelea kutoa.
Source: W Radio Colombia

RAIA WA COLOMBIA AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA