Raia wa Kenya waishio nje ya nchi yao wapiga kura leo. Sisi Tanzania tuige huu utaratibu

Raia wa Kenya waishio nje ya nchi yao wapiga kura leo. Sisi Tanzania tuige huu utaratibu

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Raia wa Kenya walioko Tanzania wamekuwa wakijitokeza kwa mafungu katika ofisi za ubalozi wao kwa ajili ya kupiga kura huku baadhi wakisifu mpangilio mzuri uliowekwa.
Ingawa kituo cha upigaji kura kilifunguliwa tangu saa moja asubuhi, lakini wengi wao walianza kumiminika kuanzia saa mbili asubuhi. Hii ni mara ya pili kwa raia wa Kenya walioko nje ya nchi kupiga kura.

Kabla ya kuingia kwenye eneo la upigaji kura,raia hao hukagua majina yao na kisha kuelekea kwenye mstari.
Kumekuwa na hali ya utulivu huku askari polisi wakipita huku na kule kuimarisha ulinzi.
 
Maendeleo ni hatua tu tutafika huko tuu
 
Democracy ya Kenya huwezi kulinganisha na maigizo yetu ya democracy ............... sisi tubaki tu kujisifia ni kisiwa cha amani wakati wenzetu wanasonga mbele!!
 
Katika historia imewahi tokea wakati wa bunge la katiba.Wajumbe waliokuwa hijja waliwahi piga kura wakio huko ili kutimiza akidi iliyotakiwa.Waliwezaje?Tunaweza kuanzia hapo...
 
Ukiona CCM wamekubali hii kitu jua tayari washapata option ya kuchakachua kupitia upande huo. Kama hapahapa nchini Total ya waliojiandikisha baadhi ya majimbo unakuta ni 40 elfu, then ukijumlisha walipiga kura unapata 75 elfu vipi itakuwaje huko kwenye balozi ambapo kimsingi wasimamizi ni wanachama watiifu wa ccm? kweli ni changamoto kwetu. kama waliweza kuchakachua kura za mashehe waliokuwa kwenye bunge la katiba, urais hatuponi. Watapiga kura watu 100 then tutaambiwa zimepigwa 100,000. na hapo ndo utaelewa how technically they (ccm) are.
 
Katika historia imewahi tokea wakati wa bunge la katiba.Wajumbe waliokuwa hijja waliwahi piga kura wakio huko ili kutimiza akidi iliyotakiwa.Waliwezaje?Tunaweza kuanzia hapo...
Nimependa neno akidi R.I.P Sitta
 
Sio lazima kuiga kila kitu, Utaja iga kugongwa mzambwanda mtoto wa kiume. Time will come and tutafanya yetu @ our right time.. Ila sio kuiga iga tu kila kitu sbb fulani kafanya, hizo akili za nyumbu..
 
Raia wa Kenya walioko Tanzania wamekuwa wakijitokeza kwa mafungu katika ofisi za ubalozi wao kwa ajili ya kupiga kura huku baadhi wakisifu mpangilio mzuri uliowekwa.
Ingawa kituo cha upigaji kura kilifunguliwa tangu saa moja asubuhi, lakini wengi wao walianza kumiminika kuanzia saa mbili asubuhi. Hii ni mara ya pili kwa raia wa Kenya walioko nje ya nchi kupiga kura.

Kabla ya kuingia kwenye eneo la upigaji kura,raia hao hukagua majina yao na kisha kuelekea kwenye mstari.
Kumekuwa na hali ya utulivu huku askari polisi wakipita huku na kule kuimarisha ulinzi.

Hapa ndipo low IQ yetu Waafrika ilipo, nchini kwetu tu kuna watu wanashindwa kupiga kura na wengi hilo hatujalitatua unataka tuanze kushughulika na watu waishio nje ya nchi tena walioondoka kwa hiari yao, hii ni ajabu sana na hiyo gharama nani atalipa?
 
Hata kabla ya hayo yote, tume huru ya uchaguzi ndo jambo la msingi. Haya mengine ni nyongeza tu!! It's not a "live or die"
 
Back
Top Bottom