Raia wa Tanzania wadakwa na mabilioni nchini Malawi

Raia wa Tanzania wadakwa na mabilioni nchini Malawi

Wachomwe na nani mkuu. Hiyo ni drama tu baadaye utaambiwa wamehojiwa ikaonekana pesa nilikuwa zinaletwa nchini ili zilipe waandamanaji.
Inaweza kuwa kweli lakini kwa Polis wetu hawa na tukio lilopo mbele sidhani. Hii inawezakana asilimia kubwa ikawa drama.
 
Igizo la CCM hilo na tawi lake la TISS-CCM na Mwigulu Nchemba
Yuko wapi yule Mjeda wa USA aliye kamatwa mpakani- Sirali,anaingiza Nchini Mabomu ya Atomiki, wakawa wanampiga picha akiwa chini ya Ulinzi,mara kwenye Toyota Cabin,Fuso,Ofisini,mara ana suti,mara Kombati...Mtu yule yule mmoja?!!!
CCM ni hatari sana.
 
Malawi wamechomwa na waliofanya biashara nao Lilongwe hapo wamepoteza mzigo bure na hela inarudi kwa mnunuzi hakuna kizuizi chochote huko wapo busy kukagua gari inayotoka zaidi zaidi watakupa salamu ya mulibwanji bhamdala...
Sababu ya pili wadogo wanaweza wakawa wamejichomesha ili wawagawie polisi kiasi huku kesi ikiwa ubaoni wao wanapata dhamana na kusepa kama ambavyo ililipotiwa jamaa alikamatwa na gari ya moto Msumbiji kumbe kajichomesha ili adhurumu tu..
Tatu inawezekana kweli wamekamatwa ila sio kwa kukagua gari hapana ni kwa mtu aliewachoma huko Lilongwe akawaacha wafike mbali ili kupoteza maboya..
 
Yeah, your suspicion may be true. Kwa umri wao sidhani kama wana akili ya kufanya “deal chafu” zenye michongo ya kuingiza kiasi hicho cha pesa
Tena wanavyoonekana kwa muonekano tu ni kama walipewa mzigo wakaambiwa wasijaribu hata kuangalia kilichomo hadi wafikishe kwa muhusika..

Kama ni wafanya biashara waliowatuma (maboss wao) hao madogo nao washamba tu.. mzigo kama huo tupia kwenye cold wallet ya crypto, unatembea na kidude kama Flash Disk lakini pesa zipo humo...

Au unawaambia nipeni cash kiasi fulani na kinachobaki wekeni kwenye crypto..
 
Naona watu wanashauri eti wange weka Kwa mfumo wa crypto wakifika huku wazitoe kiwepesi tu, tunasahau kama hizo pesa ni nyingi wangebanwa wathibitishe uhalali wa hizo pesa, huoni bado ilikua ngumu
 
Raia wawili wa Tanzania, Paschal Nyanda (28) na Sanda Donald (24), wamekamatwa na Jeshi la Polisi nchini Malawi baada ya kukutwa wakimiliki US$1,141,215 (zaidi ya Shilingi bilioni 3 za Kitanzania) bila kuwa na nyaraka zinazoonyesha uhalali wa fedha hizo.

Kwa mujibu wa Polisi, tukio hilo lilitokea Julai 1, 2026 katika kizuizi cha barabarani cha Chiweta, wilayani Rumphi, wakati wa operesheni maalumu ya ukaguzi.

Watuhumiwa walikuwa wakisafiri kwa gari aina ya Mazda Axela wakitokea Lilongwe kuelekea Tanzania, ambapo baada ya ukaguzi, askari walibaini fedha hizo zikiwa zimefichwa ndani ya gari.
Inadaiwa watuhumiwa walishindwa kuwasilisha nyaraka zozote zilizoruhusu umiliki wa kiasi hicho kikubwa cha fedha za kigeni.

Polisi wamekamata fedha hizo pamoja na gari lililotumika, huku watuhumiwa wakitarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kumiliki fedha za kigeni bila nyaraka halali na utakatishaji wa fedha baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

Instinct zinananiambia kuwa wametumwa na akina Mwigulu, ili baadaye wahalalishe kauli zao.
 
Hao madogo ni wachimbaji na hiyo "kibunda" wameipiga kibabe kwenye masuala ya uchimbaji.

Nawaelewa sana watoto wa kisukuma walivyo shapu kwenye mambo ya kiapolo wanapofumania "pocket" huwa hawalazi damu. "Afe mmasaai au mchina lazima mzigo tuchomoke nao!"

Hao wamechomwa na wachimbaji wenzao coz ni either hayo madini walipata kwa kuwazunguka wenzao au walikuwa wamefuma chimbo/mkanda wakawa wanakula wao tu kimyakimya pasipo kuonesha wenzao so wamechimba wakapata huo "mpunga" wakaona ni mwingi sana so better wauvushe TZ kwanza then watarudi tena kuendelea kuchimba ikiwa wangefanikiwa kufika nao salama.
Hivyo wamechomwa na tajiri aliye nunua madini coz hawaku disclose wapi wanachimba huo mzigo.

Msiwaone wapo cool hivyo, wanajua fika kwamba hata wakipokonywa huo mpunga chimbo bado lipo watarudi tena kupiga nyingine.

Trust me hii haihusiani na mbanga za politics. Isipokuwa madogo hawakuwa na a,b,c za kuvusha huo mpunga kimya kimya bila kudakwa. Ila ni wa kwao kabisa wamepiga kutokana na madini.
 
Malawi wamechomwa na waliofanya biashara nao Lilongwe hapo wamepoteza mzigo bure na hela inarudi kwa mnunuzi hakuna kizuizi chochote huko wapo busy kukagua gari inayotoka zaidi zaidi watakupa salamu ya mulibwanji bhamdala...
Sababu ya pili wadogo wanaweza wakawa wamejichomesha ili wawagawie polisi kiasi huku kesi ikiwa ubaoni wao wanapata dhamana na kusepa kama ambavyo ililipotiwa jamaa alikamatwa na gari ya moto Msumbiji kumbe kajichomesha ili adhurumu tu..
Tatu inawezekana kweli wamekamatwa ila sio kwa kukagua gari hapana ni kwa mtu aliewachoma huko Lilongwe akawaacha wafike mbali ili kupoteza maboya..
Wa Mwigulu hao
 
Bilion 3

Wangefika Bongo wafanye fujo na 1 B kuaminisha maskini sisi wao n matajiri wa kutupa.

Then wanafungua kampuni ya kukusanya pesa kwa raia kwa lengo lakuja warudishia mara 3 ya uwekezaji wao.

Wanapiga tena zaidi ya Bilions of money... Maisha hayaaa
 
Raia wawili wa Tanzania, Paschal Nyanda (28) na Sanda Donald (24), wamekamatwa na Jeshi la Polisi nchini Malawi baada ya kukutwa wakimiliki US$1,141,215 (zaidi ya Shilingi bilioni 3 za Kitanzania) bila kuwa na nyaraka zinazoonyesha uhalali wa fedha hizo.

Kwa mujibu wa Polisi, tukio hilo lilitokea Julai 1, 2026 katika kizuizi cha barabarani cha Chiweta, wilayani Rumphi, wakati wa operesheni maalumu ya ukaguzi.

Watuhumiwa walikuwa wakisafiri kwa gari aina ya Mazda Axela wakitokea Lilongwe kuelekea Tanzania, ambapo baada ya ukaguzi, askari walibaini fedha hizo zikiwa zimefichwa ndani ya gari.
Inadaiwa watuhumiwa walishindwa kuwasilisha nyaraka zozote zilizoruhusu umiliki wa kiasi hicho kikubwa cha fedha za kigeni.

Polisi wamekamata fedha hizo pamoja na gari lililotumika, huku watuhumiwa wakitarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kumiliki fedha za kigeni bila nyaraka halali na utakatishaji wa fedha baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

Pesa ya chadema kutoka kwa wazungu kugharamia maandamano. Shame!!
 
Back
Top Bottom