JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Vikosi vya Ulinzi na Usalama kisiwani hapa, vimewakamata raia wawili wa Uganda walioingia kwa kutumia usafiri wa jahazi katika Bandari ya Wete ambapo wamewekwa karantini maambikizi ya Ugonjwa wa Ebola.
Kamati ya Ulinzi ya Ulinzi na Usalama MKoa wa Kaskazini Pemba imefika katika Bandari ya Wete na kuwataka manahodha wa vyombo kuchukua tahadhari kwa abiria wanaowapakia.
Akizungumza katika bandari hiyo Oktoba 6, 2022, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa huo, Salama Mbarouk Khatib aliwataka mabaharia na Wananchi kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Ebola ambao umeshapoteza watu nchini Uganda.
Daktari Dhamana Wilaya ya Wete, DK. Mbarouk Suleiman Hamad amewataka mabaharia kuwa makini dhidi ya abiria wanaowachukua kujiepusha kupata aambukizi.
Raia hao wa Uganda ni Kagola Heribery na Mawanda Verai ambao waliingia Nchini kupitia mpaka wa Mtukula kwa lengo la kwenda Wilaya ya Micheweni.
Chanzo: Uhuru