Kituo cha Rwampara kilichomwa moto na vijana wenye hasira wakati wakijaribu kuchukua mwili wa rafiki yao aliyedhaniwa kufa kwa Ebola, kwa mujibu wa ushahidi wa mtu mmoja aliyezungumza na shirika la habari la Associated Press.
Naibu Kamishna Mwandamizi Jean Claude Mukendi, ambaye ni mkuu wa idara ya usalama wa umma katika eneo Ituri, alisema vijana hao walikuwa hawajaelewa taratibu zinazopaswa kufuatwa wakati wa kuzika mtu anayehisiwa kufa kwa Ebola.
"Familia yake, marafiki, na vijana wengine walitaka kupeleka mwili wake nyumbani kwa ajili ya mazishi, ingawa maelekezo kutoka kwa mamlaka wakati huu wa mlipuko wa virusi vya Ebola yapo wazi," alisema Mukendi. "Miili yote lazima izikwe kulingana na kanuni zilizowekwa."
Hama Amadou, mratibu wa shirika la kibinadamu la ALIMA ambalo lilikuwa na timu zikifanya kazi kituoni hapo, alisema baadaye kuwa hali ya utulivu imerejea na timu za misaada zinaendelea na kazi zao kama kawaida.
Hali hiyo ya hasira ya ghafla ilidhihirisha wazi changamoto kubwa zinazozikabili mamlaka za Kongo pamoja na mashirika mbalimbali ya misaada yanayojitahidi kudhibiti mlipuko huo, ambao Shirika la Afya Duniani (WHO) limeutangaza kuwa dharura ya afya ya jamii inayohitaji uangalizi wa kimataifa.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, kuna vifo vinavyohisiwa kufikia 148 na visa vinavyohisiwa karibu 600, huku visa viwili vikiwemo kifo kimoja vikiripotiwa katika nchi jirani ya Uganda. Hata hivyo, mkuu wa WHO amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa mlipuko huo ni mkubwa zaidi ya inavyoripotiwa
Soma pia
Source: Associated Press

- Uganda yakabiliana na Mlipuko wa Ebola, Watu 100+ wamewekwa Quarantine
- TAHADHARI: Ugonjwa wa Ebola Walipuka DRC na Uganda, WHO Yatangaza Hali ya Hatari (PHEIC)
Source: Associated Press