Sitegemei ukawa ya Kenya(NASA) nayo itakuwa lege lege kama itashinda na kuruhusu unyang'anyi wa ushindi wao huku ikitegemea wanainchi na huruma kutoka nje ya nchi.
Pamoja na hali ya kutoelewana wakati wanatafuta mgombea kiasi cha kuwagawa Luhya ambao ndio wana kura nyingi kwa NASA, lakini hadi kufikia mwezi wa nane huo mgawanyo hautakuwepo na badala yake wote watakuwa timu NASA.
Kuna nimeona wanajaribu kulinganisha huu uchaguzi na ule wa 2007 na kusema matokeo hayatakuwa tofauti niseme tu huu muungano wa sasa hivi haukuwepo kipindi kile na pia siasa zimebadilika.